RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.07.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOHUBIRI KATIKA IBADA YA KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU SIKU YA JUMAPILI

Tunamshukuru sana Mungu kwa ibada ya KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 30.07.2017. Mungu alimtumia Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kutulisha chakula cha uzima cha kujenga mioyo yetu na kuchoche imani zetu kuimarika. Pia alipata nafasi ya kuombea vifaa vya kupigia magoti wakati wa kuomba majumbani mwetu. Vifaa hivyo ni kama khanga, vitenge, makapeti, vibao, vitambaa n.k. Kila mmoja alileta kile anachoona kitamsaidia kupigia magoti wakati wa kuomba. Vifaa hivi vitatumika kama daraja au kiunganishi kati ya madhabahu ya Mungu na madhabahau za majumbani mwetu.

Alisema, sio kila wakati watu wanakuwepo kanisani kuomba, kuna wakati wanakuwepo majumbani mwao, na wanahitaji kuomba katika madhabahu yenye uwepo wa Mungu, kwahiyo kwa kupitia maombi ya KUUNGANISHA madhabahu hizi mbili itakuwa ni rahisi sana kuona nguvu za Mungu katika nyumba vyetu vya ibada za nyumbani.

Ibada hili ilikuwa ya tofauti sana, watu wengi waliweza kufunguliwa kutoka katika mateso yaliyokuwa yakiwaandama kwa kipindi kirefu.

Tukiwa katika maandalizi ya somo la Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, sasa tungependa kukualika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Mungu ataongea na wewe na kukuondoa katika tope la umaskini na kukuweka katika ulimwengu wa mafanikio ya kimwili na kiroho. Unatakiwa kuwa na IMANI na KUTII yale ambayo watumishi wa Mungu watakuagiza siku ya Jumapili hii.

Mungu wetu ni Mungu wa vitendo, kwahiyo Jumapili hii atakutendea na utashangaa kuona maisha yako yakianza kubadilika. Mungu wetu ni Mungu wa huruma kwa kila mtu na hasa wale anaoona wapo tayari kumtumikia wakati wote.

Yawezekana umeteseka sana katika ndoa yako, kazi yako, miradi yako, ofisi yako, mahusiano yenu, afya yako, masomo yako, biashara yako n.k kwa kipindi kirefu, leo hii nataka kukuhakikishia kuwa Jumapili hii Mungu ataingilia katika katika maisha yako na kukutetea.

Unatakiwa kuwa na upendo, kusaidia wengine, kushiriki ibada, kusoma sana Neno la Mungu, kutenda mema, kuungama dhambi zako, kuliishi Neno la Mungu, kuwa mtoaji kanisani, kushika na kuzitendea haki amri kumi za Mungu n.k ndipo utaona mkono wa Mungu ukigusa a ndoa yako, kazi yako, miradi yako, ofisi yako, mahusiano yenu, afya yako, masomo yako, biashara yako n.k

Karibu kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B", usafiri ni bure kuanzia kituo cha Mabasi Cha Makumbusho au Mwenge kwe Mataa utaona magari yetu. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Ubarikiwe na BWANA...


























































Comments