MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTUMISHI WA GOSPEL KUPITIA HIP HOP DP DOUGLAS ALIA NA KILICHOMKUMBA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI MUSA SHABANI NA KUPOTEA KATIKA ULIMWENGU WA GOSPELMussa Shaban.
Huyu ni kijana muimbaji wa muziki wa injili alifanya vizuri sana na nyimbo zake kama msaidizi na ushuhuda.nasikitika kuwa kipaji hiki kimepotezwa au kinaangamizwa na watu kadhaa akiwemo mgeni rasmi wakati wa uzinduz wa album yake. Kijana amejeruhiwa sana Tena na mambo mengi yaliyomkatisha tamaa kwenye uimbaji .kuanzia meneja wake wa kwanza presenters na mgeni rasmi . ivyo nyie wageni rasmi ni bora umwambie MTU siwezi kuwa mgeni rasmi wako kwa sababu ya kiuchumi kuliko kufika kwenye tukio alafu mna sema mtatoa kiasi kadhaa mamilioni alafu ikifika muda wa kutimiza kile mlichosema mtatoa mmekuwa waongo na magumashi mengi njoo kesho nyingi nitakupigia nyingi mwisho wa siku MTU anakata tamaa .Bahati mbaya Jamii inakua inajua we umepata hela kumbe hola .mtu anafatilia hela kwa mgeni rasmi kuna wakati inamlazimu kutembea kwa miguu kwa ajili ya kufatilia Pesa kwa mgeni rasmi na kushinda njaa.akifika atakalishwa foleni Ofisin kwake mwisho wa siku unaambiwa boss kasema njoo kesho Leo ana wageni .shubamiti zenu yani umemuweka MTU kwenye benchi ofisini kwako toka saa mbili asubuhi saa kumi jioni ndio unamwambia aje kesho? Mungu anawaona.kwa kifupi mtu anapofanya uzinduzi uwa na mipango mingi ya kihuduma japo wengine wanakua na mipango ya njaa kidaka tonge.sasa kwa mwenye mipango ya Huduma uwa mnawarudisha nyuma sana coz wanakua wamewekeza visent vyao kwenye uzinduzi wakitarajia baada ya uzinduzi kile watakachokipata kwenye uzinduzi jumlisha na cha mgeni rasmi kiwasukume kwenye Huduma Matokeo yake wageni rasmi mnazingua.mmewarudisha nyuma watu wengi sana pasipo nyie wenyewe kujua na amini kuna siku mtalipwa sawa na mnavyowazungusha watu.mi ni mmoja wapo kati ya watu ambao mgeni rasmi kaniangusha ipo siku nitaelezea kwa Leo ngoja Nile korosho nakushushia na soda.kuna waimbaji wengi sana ni kama wamedhulumiwa na wageni rasmi .nyie wageni rasmi ni bora muwe mnasema mtatoa Pesa ndogo mtazoweza kutoa kuliko kuwasumbua watu kwa ahadi zenu hewa. 

Na nyie waimbaji muache kuwalazimisha watu kuwa wageni rasmi kwenye event zenu maana dah na nyie mmezidi kubwa kero mkiona MTU alikua mgeni kwa muimbaji Fulani na aka ahaid milioni kadhaa basi kila muimbaji atamtafuta hiyo huyo hili awe mgeni rasmi wake hata akimwambia nitakuwa sipo nimebanwa utasikia hooo utatuma mwakilishi nyie waimbaji Mungu anawaona mjue.kina waimbaji wao kazi yao kutembea kwenye makanisa na kuangalia mshirika yupi aliyenona hili ampige shubamiti ole wenu siku mnifate mie na hivi nilivyo na mwili wa kibosi bosi mkithubutu kunifata HAKI ya nani nitafanya kitu alichofanya yesu pale hekaluni yerusalemu nawabidua bidua alafu nawapa za chembe za kiroho .nasema hivi muache tabia hizo.Mdogo wangu Mussa Shabani najua sasa umerudi upya kwenye muziki wa injili nami nakuombea Mungu ufanye kazi ya Mungu kwa kiwango kikubwa tukuone kwenye huduma makanisani na kwenye matamasha kama zamani ikibidi zaidi ya zamani.achana na hawa wagema urimbo ambao kazi yao nikurudisha watu nyuma kwa vineno vyao na dharau.dah naona povu linanitoka kweli acha Nile korosho za Mtwara nakumung'unya mung'unya na Pepsi baridiii.

KIDONGE HIKI MWENYE KUMEZA AMEZE MWENYE KUTEMA ATEME.
UKIRUHUSU WAKUJUE SANA WATAONGEZEA NA YA KWAO.

SOURCE: 
0