RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09,09.2017: WATU WAKIMBILIA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KUBATIZWA NA KUISHI MAISHA YA WOKOVU

Siku ya Jumapili 03/09/2017 katika ibada ya HABARI NJEMA iliyofanyika ndani ya hekalu la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linaloongozwa na mmbeba maono Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mbunge) kulikuwa na ubatizo wa maji mengi kwa watu waliokoka siku hiyo. Tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mungu kwa kuwaokoa mamia ya watu waliofika katika madhababu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa na hamu ya kuongozwa sala ya toba, kuombewa, kubatizwa kwa maji mengi, kupokea Roho Mtakatifu na kujifunza Neno la Mungu kwaajili ya kuwasaidia katika maisha mapya ya wokovu.

Pia tuna kila sababu ya kuwashukuru watu wote waliowatia moyo na kuwaleta kanisani watu hawa ili waokoke. Mungu atawalipa kwani kazi mliofanya ni kubwa sana, mmeokoa roho za watu kutoka kwenye shimo la dhambi.

Katika zoezi la kubatizwa, baadhi ya waongofu wapya walianaza kutokwa na mapepo wakiwa katika basi la kanisa wakielekea katika eneo maalum la kuwabatizia hawa waongofu wapya. Na baada ya kufika eneo la kushukia (kituo), watu walizidi kutokwa na mapepo na wengine kuangaka chini huku wakikataa kwenda kubatizwa. Tunawashukuru sana wainjilisti, wachungaji na wahudumu wote kwa msaada mkubwa walioutoa kuwasaidia hawa waongofu wapya ili waweza kufika katika eneo la maalimu la kuwabatizia.

Kipindi wanabatizwa wengi wao walianza kupiga kelele kutokana na moto wa Yesu uliokuwa ukiwaka ndani yao na kuunguza mapepo, huku wengine wakijazwa Roho Mtakatifu. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa wahuduma kuwasaidia hawa waongofu wapya ambao wengine walikuwa wakikimbia huku kule wakihangaishwa na nguvu za giza zilizokuwa zikipambana na Nguvu za Mungu.

Pia wengi wao walianza kunena kwa lugha kutokana na nguvu za Mungu zilivyokuwa zikifanya kazi ndani ya miili yao huku wakijazwa Roho Mtakatifu.

Baada ya ubatizo waumini waliekea kanisani kwaajili ya kubadilisha mavazi yao, kupata chakula na vinywaji na kusalimiana wa wachungaji wa kanisa hilo.

Siku ya Jumatatu na Jumanne ni skiu zao za kuanza masomo ya kukulia wokovu ambayo yanaanza saa 9 mchana na kuendelea.

Sasa, tunakuomba sana katika maombi yako unayoomba, usisahau kuwaombea watu hawa ambao ni waongofu wapaya ili wazidi kudumu katika wokovu. Kipindi hiki kwao ni kipindi kigumu sana kwani shetani naye anajitahidi kuwawinda ili warudi nyuma walikotoka. Maombi yako yatasaidia sana kuokoa Roho za hawa ndugu na jamaa zetu. Kila unaomba maombi yako usisahau kuwakumbuka watumishi hawa. Kumbuka hata wewe ulivyookoka kuna watu walitenga muda wao kukuombea na ndio maana umedumu katika wokovu na uafurahi mafanikio kimwili na kiroho unayoyapata.

Pengine wewe unayesoma hujaokoka na ukngetamani sana kuokoa, nafasi bado ipo. Jumapili hii tutawaombea na kuwabatiza waongofu wapya kwahiyo jitahidi kuwahi kanisani. Ibada inaaza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Jinsi ya kufika kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B". panda magari yatakayofika kituo cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Ukifika hapo utaona magari yetu. Ingia humu na hautaripia nauli, na baada ya ibada kumalizika utarudishwa kituo.





























































Comments