RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

AMBWENE MWASONGWE ATOA UJUMNBE MZITO SANA, ASEMA, " USIDANGANYWE NA RANGI NZURI"

Wakulima watanielewa zaidi, waweza ona rangi ya EMBE kwa mbali ukadhani limeiva, ni mpaka ulisogelee, ULIMINYE ukiona gumu jua bado bichi, USILICHUME, lipe muda LIKOMAE NA LIIVE ndipo lichumwe ama lidondoke na kushuka chini lenyewe kuyaachia nafasi mengine kutungwa,na kuwa chakula ama tunda zuri tayali kwa kuliwa. 

Natumia mfano huu kueleweka hasa kwa waimbaji wanaotamani ama wana ndoto za kuingia kwa huduma hii, WASIDANGANYWE NA RANGI NZURI ( sauti nzuri, uwezo wa kwenda studio nk) WAKADHANI WAKO TAYALI KWA HUDUMA. Subirini kuminywa( Kuhakikiwa) ama Kushuka chini ( kunyenyekezwa) ili muwe waimbaji bora na wenye matunda mazuri kwa walaji wenu. 

Nasema haya maana nimeshapitia huko, hakuna neno nilikuwa silipendi na nililolichukia kama SUBIRI MUDA WA MUNGU, Niliona kama nacheleweshwa, naonewa wivu, hawapendi mafanikio yangu, hawataki niinuke nk. 

Leo nakuudhi na wewe kwa neno hilohilo,( ila kwa upendo mkubwa) SUBIRI MUDA WA MUNGU, SUBIRI KUMINYWA, SUBIRI KUSHUKA. NDIPO UTAKUWA TAYALI. Maana wengi mnadhani mafanikio yenu na hatima yenu iko kwa waimbaji wakongwe, ama kwa kuhitaji wawashike mkono, ama kufanya nao collable ndipo mfanikiwe, Mnajidanganya kabisa tena nawavunja moyo kwa upendo kabisa. 

Subiri muda, usidanganywe na mazingira, na watu, na sauti nzuri, na uwezo wa kwenda studio, ndio maana wale wanaonekana wamefanikiwa si kweli kwamba wanaimba vizuri, si kweli kwamba wana sauti nzuri LA hasha wamekutana na Neema na wakati wao sahihi, nawe subiri ili uponywe na KIBURI, NA MANUNG'UNIKO, 

KAMA UMEITWA UTASUBIRI MAANA SAA YAKO IPO, KAMA HUJAITWA USIJIITE MAANA UTAVUNJIKA MOYO SANA, PIA OMBA MUNGU AKUPE KIBALI UTAMUONA AKIKUINUA NA UTUKUFU ATAPEWA MUNGU, SI KWA COLLABLE WA MWIMBAJI MKONGWE, ASOMAYE NA AFAHAMU


Comments