RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MANENO MAZITO KUTOKA KWA MWIMBAJI WA GOSPEL NEEMA MUDOSA KWA WASICHANA WALIOCHELEWA KUOLEWA




Nani kakwambia kwamba ukiwa na miaka zaidi ya 35 huwezi ukafanya chaguo nzuri?ao ukapata mtu unae mtaka ?#Unaweza

Dada Nani kakwambia kwamba kwakua umezaa ujichukie sasa na kufungua mlango kwa kila ane gonga,na kukubali kwa kila aitae?umezaa watoto ao mtoto ila bado una mimba ya ndoto zako ,elewa kwamba kuzaa sio mwisho #RELAX

Sio kwa sababu hujasoma ndio huna thamani mpendwa wangu,thamani yako iko pale pale,usiji zarau na kushindwa kua na maamuzi .Mungu amekupa akili na inatosha kukufanya Uishi kama wengine. ondoa complexe .unaweza💪


Yawezekana umezaliwa kwenye familia maskini na unaishi kwa kujikataa mwenyewe.hujuwi kusema hapana kwa watu wanao kusaidia,umejitupa kwenye mahusiano yasio julikana ili tu maisha yaende .NON NON NON STOP
Wengi unao waona walianza chini zaidi kuliko hata wewe ila hawakukata tamaa,walimwamini Mungu,wakasimama na Mungu,na leo wako juu maana Mungu huwachukua walio chini na kuwaweka juu,#TULIA hata kwako atatenda

a)usipo jipenda hakuna atakae kupenda
b)usipo jikubali hakuna atakae kukubali
c)usipo jiheshimu utasubiri saana heshima toka nje
d)usipo jithamini hakuna atakae kuthamini

Ungejua ni jinsi gani Mungu anavyo kupenda na kukuthamani ungeji thamini zaidi

Comments