RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.11.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA IBADA YA KUVIKWA KIBALI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

//Zaburi 16:1-3: Mungu, unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe. Nimemwambia BWANA, ndiwe BWANA; sina wema ila utokao kwako. Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao//

siku ya Jumapili 19.11.2017katika ibada ya KUVIKWA KIBALI ilikuwa ni siku ya baraka sana, watu wengi walijitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa na kiu ya KUOKOKA . Mch. Rosemary Mgetha aliwaongoza sala ya toba, wakaombewa na baadae kubatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku yao ya kuanza mafundisho ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.


Pengine ungetamani kuokoa na kupokea Yesu kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Tunawkaribisha wote.

Mch. Rosemary Mgetha




















 




























Comments