RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.11.2017: WATU WAKIMBILIA BARAKA ZA SHILO KATIKA MADHABAHU YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

// WHAT You are Able to DO in the NAME OF JESUS depends on YOUR capacity to BELIEVE. Mathew 11:20//

Hivi ndivyo watoto wa Mungu walivyoweza kukusanyika kwa pamoja na kuonyesha uzalendo na ile hamu ya kumtafuta Mungu. Hii ilitokea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 19.11.2017 kwenye ibada ya KUVIKWA KIBALI ambapo watu walijitokeza katika madhabahu ya kanisa hilo kwa lengo moja la kuchota baraka za Mungu kwa kujitolea kusapoti kongamano la SHILO TANZANIA litakaloanza Jumapili 03 hadi Jumapili 10. Desemba. 2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Huu ni upendo wa ajabu sana, kwani kitendo cha kusapoti kongamano hili, inamaanisha watu hawa wamethamilia kuokoa roho za watu zinazoteseka na kuhangaishwa na shetani kwa njia mbalimbali. Kamati ya maandalizi kwa heshima na taadhima iliwagawia bahasha waumini na wageni waliofika madhabahuni kwaajili ya kujichotea baraka zao zitakazotokana na UTOAJI.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude amekuwa mstari wa mbele akiwaombea watu wote wanaojitoa kusapoti kongamano hili na pia wale wanaojitoa kwa mali zao, elimu zao, vipaji vyao, huduma zao kwaajili ya SHILO.

Kongamano hili litakuwa likianza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana kwa siku za Jumapili, na siku za katikati ya wiki litakuwa likanza saa 9 mchana hadi saa 1 usiku.

Wahubiri wa kongamano hili ni Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Pastor paul Kuria kutoka Kenya, Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha, Mch. Elias Madoshi (shinyanga), Mch. sylavanus Komba (Dodoma) na wengine wengi.


Tunakukaribisha sana.

Kamati ya Shilo Tanzania 2017 Mlima wa Moto Mikocheni "B"


































Comments