RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FANYA KILE UNACHOKIPENDA

Rulea Sanga

Je, unachokifanya unakipenda? Kama hukipendi basi achana nacho kitakupotezea muda wako. Muda ni muhimu sana. Usifanye kitu kwa kuiga wakati wewe mwenyewe hukipendi, mwisho wa siku utaishia kujilamu pale utakapoona ulikuwa unapoteza muda wako.

Unajua kila kitu hapa duniani kina mwanzo na mwisho kwahiyo hicho unachofanya ujue kuna mwisho wake, sasa angalia mwisho wake kama utakusaidia au utakufanya ujilaumu kwa ule muda uliokuwa unaupoteza kwa kufanya kitu usichokipenda.

Kama mtu atakushauri kufanya kitu usichokipenda, na ukaona yeye amefanikiwa kupitia hicho usichokipenda kukifanya, muulize Mungu akupe hekima na maamuzi sasa ili baadae usijijutie..Mungu ni mwema atakupa majibu sahihi kwa wakati sahihi...

Usikate tamaan kumuulize Mungu akupe kile unachotaka kukifanya ili ufanye kwa kupenda na ufanya kwa bidii zako zote ...Kithamini unachopenda kukifanya na ili kikuthamini hapo baadae... "Mungu ni mwenye huruma"

Comments