MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

05.12.2017: BAADHI YA WATU WALIOJIUNGA NA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KATIKA KONGAMANO LA SHILO 2017

Hawa ni baadhi tu ya watu walioamua kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumanne 05.12.2017 katika kusanyiko la watoto wa Mungu la SHILO ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Na mwaka huu lilifanyika kuanzia tarehe 03 hadi 10.12,2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Wanenaji walikuwa ni wengi sana na baadhi yao ni Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Paul Kuria kutoka Kenya, Mch. Noah Lukumay, Mch. Sylvanus Komba, Mch. Elias Komba na wengine wengi. Ilikuwa ni siku ya BWANA Kujifunua katika maisha ya watu (1 Samweli 3:21) na pia watu kufunguliwa katika mateso wanayopitia. Hakika Mungu alionekana kwa namna yake, watu waliguswa na nguvu za Mungu isiyo ya kawaida.

Sasa, tunakukaribisha na wewe ambaye unatamani kujiunga na huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Fomu za kujiunga zinapatikana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tu na katika matawi ya makanisa ya Mlima wa Moto Tanzania. na siku ya Jumapili hii kutakuwa zitatolewa fomu kwaajili yako wewe unayetamani kujiunga na huduma ya Mlima wa Moto. Mungu na akubariki sana.
 Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
0