RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.12.2018: MCH. PRISCA CHARLES ALIVYOONGOZA KIPINDI CHA SIFA KATIKA IBADA KUSHIKWA MKONO NA MUNGU

BWANA anasema katika kitabu cha  Zaburi 2:8, "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urith wako, na mmisho ya dunia kuwa milki yako"
Kumbe Mungu ametupa kibali cha kumuomba ili tuweze kupewa mataifa yote kuwa urith wetu. Unayo nafasi ya kumuomba Mungu wetu lolote naye atakupa, unachotakiwa ni kufuata maagizo yake na kanuni zake kupitia kitabu kitakatifu na pia kupitia watumishi wake alio Mungu kupitia kitabu kitakatifuwaweka duniani.

Katika kitabu cha Zaburi 9:11, Biblia inasema hivi, "Mwimbieni BWANA akaaye Sauyuni, yatangazeni kati ya watu matendo yake." Kwahiyo tunakumbushwa kumwimbia BWANA na kutangaza yale matendo makuu anayoyafanya kwa viumbe vyake. Kama wewe unaona umetendewa jambo na Mungu yakupasa kulishuhudia ili na wengine wainuliwe kiimani. Pia kuna njia nyingi za kulitangaza Neno la Mungu. Kwa kizazi cha sasa, unaweza kutangaza matendo makuu ya Mungu kwa njia ya uimbaji, kufundisha, kuhubiri n.k, na habari hizi unaweza kusambaza kwa watu wengi sana kwa kutumia socia media, vyombo vya habari, watu binafsi na wewe mwenyewe kwa kupita mitaani ukishuhudia matendo makuu ya Mungu yaliyofanyika kwako au kwa mwenzako.

Siku ya Jumapili 14.01.2018 katika ibada ya kushikwa Mkono na Mungu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mch. Prisca Charles aliweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji akishrikina na Praise & Worship Team, Waumini wa kanisa hili walionekana kuguswa na uwepo wa Mungu kupitia mtumishi wake Mch. Prisca Charles wakati akiimba. kanisa liliweza kutimiza agizao la Mungu. Kitendo alichokifanya Mch. Prisca Charles ni moja ya kutangaza matendo ya Mungu na pia kumsifu Mungu.

Mch. Prisca Charles
































Comments