RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.02.2018: MCH. NOAH LUKUMAY AKISHIRIKIANA NA WACHUNGAJI 12 WAFANYA MAOMBI KATIKA IBADA YA BIG SUNDAY TO REMEMBER 2018



//ZABURI 119:169 Ee BWANA, kilio changu na kikukaribie, unifahamishe sawasawa na neno lako. Dua yangu na ifike mbele zako, uniponye sawaswa na ahadi yako.//

Hivi ndivyo watu wa Mungu walivyopaza sauti zao kwa Mungu ili asikie kilio chao katika ibada ya BIG SUNDAY TO REMEMBER iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 11.02.2018. Mch. Noah Lukumay aliongoza ibada hii ya maombezi. Katika ibada hii watu wengi sana walifunguliwa kutoka katika gereza na mateso na shida. Ilikuwa ni ibada ya nguvu za MUngu na iliyotanda uwepo wa Kimungu pande zote. 

Kumbuka, Ibada hii ya BIG SUNDAY TO REMEMBER hufanyika mara moja tu kwa Mwaka na hukusanya waumini wa makanisa yote ya Mlima wa Moto Tanzania katika makao makuu ya kanisa la Mlima wa Moto yalliyoko Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam.

Siku hiyo watu waliomba dua zao mbele za Mungu na kila mtu alipeleka ombi lake kulingana na mahitaji yake. Katika maombezi hayo baadhi ya watu walitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza. Wakati watumishi wa Mungu tulishuhudia mapepo yakipiga kelele yakitaka kutoka katika miili ya watu. Na hii inatokana na moto wa Mungu uliokuwa ukiyachoma kupitia jina la Yesu.

Katika kitabu cha ZABURI 120:1 kinasema, "Katika shida yangu nalimlilia BWANA Naye akaniitikia." Kwahiyo unapokuwa na shida Mungu wetu yupo tayari kuitika kilio chako na kukufuta machozi yanayotokana na machungu au kuumizwa na majaribu au changamoto unazopitia. Kwahiyo unapokuwa katika hali ya kutokwa na machozi ya uchungu, unachotakiwa kukifanya ni kujiunganisha na mtambo wa Mungu kwa kutenda mema na kusoma Neno la Mungu ili upate siri za Mungu juu ya maisha yako. Unapomlilia Mungu kwa kumaanisha, Mungu anakuwa karibu na wewe kukusaidia, lakini kama utakuwa ni mtenda maovu na unajijua wewe ni muovu, Mungu naye anakuwa mbali na kilio chako. Kama umejigundua kuwa ni muovu, basi omba watumishi wa Mungu wakuongoze sala ya toba ili uwe karibu na Mungu Naye atakufuta machozi yako na kubadilisha historia mbaya ya maisha yako.

ZABURI 120:2, inasema "Ee BWANA uniponye nafsi yangu na midomo ya uongo na ulimi wa hila. Kama muumini uliyekamilika na uliyejiandaa kwenda mbinguni unatakiwa kuachana na tabioa ya uoongo kwa maana ulimi wako wenye hila ni sumu kubwa kwa mwingine. Uongo unaomtakia mwingine unaweza kuzaa matunda mabaya sana na kusababisha ukosefu wa amaini katika maisha yako, familia yako na taifa lako.

Sasa wewe ambaye umekuwa ukisumbuliwa na pressure, kansa, UKIMWA, vidonda sugu, Kiuno, miguu, kichwa n.k na umehangaika bila ya mafanikio, nataka nikuambie yupo Yesu mtenda miujiza anayefanya miujiza yake kupitia watumishi wake aliowakweka duniani. Unatakiwa kuwatii na kuwaheshimu watumishi wa Mungu kwani wao ni mabalozi wa Mungu hapa duniani. 

Na wewe ambaye hujapata kazi, wateja, promosheni, kibali wateja katika biashara yako, mume/mke, kiwanja, nyumba, kodi nyumba, ada ya shule n.k, nataka nikuambie ya kwamba mshikirie huyu Yesu wala usimuache katika maisha yako na utaona atakavyoanza kuachia baraka zako katika maisha yako. Utamshikiria Yesu kwa kutenda matendo mema kama anavyokuagiza katika Biblia yake, kushiriki ibada ili kuinua imani yako na kuimarisha mahusiano yako na Mungu, kufunga na kuomba, kuonyesha upendo kwa kila mtu, kujituma kufanya kazi ya Mungu, kuwasaidia wenye uhitaji, kutoa zaka na fungu la kumi kanisani, kuwaheshimu na kuwatii watumishi wa Mungu, kuzishika amri za Mungu na kuzifanyia kazi na mengine kama hayo.

Mwisho nataka kukuaribisha katika ibada ya Jumapili itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Karibuni wote.
Mch. Noah Lukumay


Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare






































xxxxxx




















Comments