RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.02.2018: PICHA ZA FURAHA ISAYA AKIIMBA KATIKA IBADA YA BIG SUNDAY TO REMEMBER MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

//ZABURI 109:1-5 "Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze, kwa maana umenifumbulia kinywa, kinywa cha mtu asiye haki cha hila, wamesema nami kwa ulimi wa uongo. Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka. Wamepigana nami bure. Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, ijapokuwa naliwaombea. wamenichukuza mabaya badala ya mema, na chuki badala ya upendo wangu.//

Yatafakari maneno haya na sikiliza wimbo wa Furaha Isaya wa unaosema "Ulinisukuma Sana Ili Niangamie lakini BWANA alikuwa upande wangu. Hivi ndivyo tulivyobarikiwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Furaha Isaya katika ibada ya Jumapili 11.02.2018 ya BIG SUNDAY TO REMEMBER iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kumbuka ibada hii hufanyika mara moja tu kwa mwaka na hukusanya makanisa yote ya Mlima wa Moto Tanzania na kufanya ibada ya pamoja na kula chakula cha pamoja. Ibada ii huchua masaa zaidi ya 12 na huanza saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Ni ibada ambayo huwa ni ya kipekee na iliyojaa nguvu za Mungu.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Furaha Isaya



















Comments