MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

18.03.2018: DADA AMSHUKURU MUNGU KWA KUMUOKOA KATIKA CHANGAMOTO ALIYOKUWA AKIPITIA

TAFAKARI
MITHALI 29:25-26. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo kwa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA.//

Dada huyu kwa machozi ya furaha alimshukuru Mungu kwa kumuokoa katika changamoto aliyokuwa akipitia ambayo hatutaitaja hapa. Mungu alimuokoa katika mateso na kumrudishie heshima yake kama awali. Hakika kuwaogopa wanadamu huleta mtego, ila yeye amtumainie BWANA katika mapito yake atakuwa katika mikono salama.

Dada huyu alimshukuru sana Mungu kwa kumuokoa katika changamoto yake na alimshukuru sana tena sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi yake ambayo hakika yameleta majibu chanya. Pia aliwashukuru wazee wa kanisa, vijana, wamama na wababa wa Mlima wa Moto kwa maombi yao.

Yawezekana unapitia changamoto fulani na umejitahidi kwa akili za kibinadamu ikashindikana. Leo nataka nikwambie kuwa yupo Yesu mtenda miujiza anaweza kufanya muujiza wako mpaka maadui zako washangae. Kuna watu wanatamani kukuona kila siku unakutwa na mabaya, unaumwa, hufanikiwi, unateseka, unakuwa mtu wa majonzi, unakosa amani n.k.

Nijiunganishe na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili hii ili ukutane na huruma na neema za BWANA katika maisha yako. BWANA atakutoa hapo ulipo na kukuweka katika viganja vyake na utakuwa salama.

Tumeshuhudia watu wengi wanafunguliwa katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B", wengi wanaokoa, wengi wanapokea baraka za BWANA, wengi wanainuliwa imani zao, wengi wanapokea mafundisho ya kukulia wokovu wao, wengi wanafanikiwa kimwili na kiroho. Njoo mtu wa Mungu ufanyike nguzo katika kuujenga mwili wa BWANA na upokee baraka zako.

Ibada inaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola - DSM.0