RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

18.03.2018: MATUKIO KATIKA PICHA YA MCH. SYLVANUS KOMBA KUTOKA MLIMA WA MOTO DODOMA AKIHUBIRI SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" -DSM

TAFAKARI:
// MITHALI 29:1. AONYWAYE mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa.//

Yawezekana umeonywa sana na watumishi wa Mungu juu ya KUOKOKA au kumtumikia Mungu lakini umeshupaza shingo yako kwa kukataa WOKOVU au kumtumikia Mungu na matokeo yake maisha yako yamevunjika au yameharibika yaani hayana mwelekeo mzuri, kila jambo kwako halifanikiwi na umehangaika kutafuta majibu kwa waganga na kwa wanadamu lakini haujapata dawa au majibu. Umebaki mkiwa, ukitaabika, ukiyumbishwa na dunia, ukilia, ukiwaza. Wale uliokuwa nao wamekutenga, unaonekana kikatuni, hufai, huna thamani mbele za watu, umekuwa ni mtu wa kuhangaika kupata uponyaji kutokana na mamgonjwa yaliyokuandama, umechelewa kuoa au kuolewa, huna watoto na umri umekwenda, huna kazi,hupata kibali kazini kwako, ndoa yako haina amani, mshahara wako umedumaa wala hupandishwi wakati wenzako wanapandishwa mishahara, kupata kodi ya nyumba kwako ni shida, kujenga ni kama ndoto kwako, kila unachogusa hakifanikiwi, mikono yako imelaaniwa, mawazo yako yanawaza mabaya tu, ukekuwa ni mtu wa kulewa, kufanya uzinzi, kufanya mabaya ambayo hayafai katika jamii, mapepo yamekuandama, umekuwa ni tapeli, kila kona wanakuwinda kwa madeni, mpangaji wako kila kukicha ni ugomvi kwa kukosa kodi, mawazo yako ni ya kujiua.

Nataka nikuambie kuwa yupo Yesu Kristo Mtenda miujiza ndani ya hekalu la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Legeza shingo yako na umrudie huyu Yesu Kristo akupe wepesi katika maisha yako, akuepushe na mabaya, akuonyeshe njia sahihi ya kufikia malengo yako, akupe mpenyo katika yale unayotamani yatokee kwako. Mungu wetu ni Mungu wa huruma na upendo, anakupenda hata kama umeathirika na maovu, anakuita njoo umpokee sasa. Mtumishi wa Mungu Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Mungu amemuweka kwaajili ya kuokoa maisha yako. Wengi waliokubali na kutii maagizo yake wamepokea MIUJIZA yao na sasa wanafurahia upendo wa Yesu Kristo. Mungu anamtumia kwa viwango vya juu sana. Mungu amembariki kimwili na kiroho.

Tunamshukuru sana mtumishi wa Mungu Mch. Sylvanus Komba kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Dodoma. Siku ya Jumapili 18.03.2018 alifanyika baraka kwa mafundisho ya kuinua IMANI za watu na kuimarisha WOKOVU wetu. mafundisho yake yaligusa sana maisha ya watu. Mungu alimtumia kwa njia ya tofauti sana na watu walionekana kuguswa na ujumbe wa Mungu kupitia kinywa chake. 
kwa sasa tupo katika maandalizi ya mahubiri yake ambayo utapa kupitia post zetu, na tutakuandalia link ya video ya mahubiri yake.

Kanisa limendaa usafiri wa bure kuanzia Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola DSM na siku ya Jumapili ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola DSM

Mch. Sylvanus Komba













































Comments