RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

18.03.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIWAPAKA MAFUTA YALIYOOMBEWA WAUMINI SIKU YA JUMAPILI

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapilli 18.03.2018 waliwapaka mafuta yaliyoombewa waumini na wageni wote waliofika kuabudu katika kanisa hilo. Baada ya kupakwa mafuta, baadhi yao waliotokwa na mapepo na kuanza kupiga kelele kutokana na moto wa Yesu uliokuwa ukiyachoma mapepo na kuyaangamiza. Unajua mambo haya yote yanaenda kwa imani. Mtu kama huna imani na tendo la kupakwa mafuta usitegemee kupokea muujiza wako. Kwanza unatakiwa kuwa na imani, pili mkumbushe Mungu kwa yale maombi yako ili akusaidie, ishi maisha ya kumpendeza Mungu kila kuitwapo leo.

Kupitia mafuta haya luna nguvu za Mungu, kupitia mafuta haya watu wanakombokewa, wanaponywa, waoa/ kuolewa, wanapata kazi, wanainuliwa, wanapata promotion, wanapandishwa vyeo, wanajenga, wananunua magari, huduma zao zinaongezeka, wanaheshimishwa, wanapata watoto, wanaponywa magonjwa sugu, wanafaulu masomo yao, miradi yao na mifugo yao inaongezeka, mashamba yao yatoa mavuno mengi n.k. Kwahiyo amini watumishi wa Mungu wanapokuelekeza kuhusu mafuta haya yaliyoombewa. Ukiyahitaji kwaajili ya matumizi yako yanapatikana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni 'B"

Sasa nikualike wewe ambaye ulikosa nafasi hii kushiriki ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Na siku za Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ibada itaanza saa 9 alasiri na usafiri utakuwepo Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

 Mchungaji kutoka Bunjumbura, Burundi



Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma




Mch. Mama Mgetha

Mch. Stanley Nnko



Mch. Victor Kutoka Kenya

Bishop kutoka Brazil


Mch. Alex Mapanga


Mch. Prisca Charles


Mch. Sunga

Mama Mshobozi

Martha Komanya












Mr. Jonathan

Comments