MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WATU WAZIDI KUFUNGULIWA KATIKA SEMINA YA KUMLINGANA MUNGU..USIPANGE KUKOSA

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na Mch. Sylvanus Komba kutoka kanisa la Mlima wa Moto Dodoma wanakualika katika Semina Ya Siku 5 ya Maombi ya KUMLINGANA MUNGU inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni mpaka siku ya Ijumaa 23.03.2018 Semina hii ilianza rasmi siku ya Jumatatu 19.03.2018 na Jumapili itakuwa ndio hitimisho

Leta hoja zako mbele za Mungu kwa siku hizi tano na Mungu atajibu sawasawa na hoja yako kwani Yule Yesu aliyetenda anaendelea kutenda hata leo, yule Yesu aliyeponya anaendelea kuponya hata leo, yule Yesu anayewainua wanyonge anaendelea kuinua hata leo. Kwa siku hizi tano ni lazima utoke na MUUJIZA wako.

Siku hizi tano ni za maombi ya KITIMUTIMU kwani huu ni msimu wa maombi na ni kipindi cha kukutana na Mungu anayejibu maombi kulingana na haja ya moyo wako. Watu wengi wanafunguliwa iweje wewe usifunguliwe wakati ni mtoto wa Mungu? Mungu wetu hana upendeleo kabisa, atakufungua na wewe, usikate tamaa bali chukua maamuzi ya kufika ibada siku ya leo.

Yeremia 33:3 na Isaya 43:26. BWANA anakwenda kuondoa udhaifu katika familia yako, kazi yako, ajira yako, ndoa yako, uzao wako, masomo yako, huduma yako, karama yako, afya yako n.k. Njoo UKIAMINI na utaona mkono wa BWANA katika maisha yako.

Kanisa limendaa usafiri wa bure kuanzia Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola DSM na siku ya Jumapili ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola DSM
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mch. Sylvanus Komba (Mlima wa Moto Dodoma)


0