RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

01.04.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOPOKELEWA KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA PASAKA

Hivi ndivyo Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alivyopokelewa na wadau wa Praise Power Radio katika tamasha la Mega Mkate na Praise Power Radio 99.3FM lililofanyika siku ya Jumatatu ya Pasaka 02.04.2018 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kenton Afrikasana Sinza jijini Dar es Salaam-Tanzania. Lengo la tamasha hili lilikuwa ni kwaajili ya watangazaji na uongozi wa Praise Power Radio kufurahi na kusherekea Jumatatu ya Pasaka na wadau wake au wasikilizaji wa radio hiyo. Na pia kuwahamasisha watu kuendelea kusikiliza PPR 99.3FM ili waweze kuinuliwa kiimani na kujifunza Neno la Mungu kupitia watumishi mbalimbali wanaohubiri na kutangaza Injili kupitia radio hiyo. Radio hii ya dini ipo chini ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na inajishughulisha na kusambaza Injili mikoa ya Tanzania na duniani kote. Radio hii pia inapatika Online kwa watu walio mbali na frequency za 99.3FM Katika tamasha hili kulikuwa na burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili, michezo ya watoto, Neno la Mungu na Maombezi. Na lilikuwa ni tamasha kwa watu wote bila kujali dini, kabila, rangi, umri, jinsia, taifa. Tamasha lilianza saa 4 asubuhi hadi saa 2 usiku.






















Comments