RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

01.04.2018: WATANGAZAJI WA PRAISE POWER RADIO 99.3FM WALIVYOONGEA NA WASIKILIZAJI WA PPR 99.3FM KATIKA TAMASHA LA MEGA MKATE

Watangazaji wa Praise Power Radio 99.3FM walivyoweza kusalimiana na kujitambulisha kwa wadau au wasikilizaji wa Praise Power Radio katika tamasha ya Mega Mkate na Praise Power Radio 99.3FM lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kenton Afrikasana Sinza jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu ya Pasaka (April. 02.2018). Mgeni Rasmi alikuwa ni Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Lengo la tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka ni kukutana na kufurahi kwa pamoja na wadau au wasikilizaji wa Praise Power Radio 99.3FM kupitia michezo mbalimbali, burudani na pia kuweza kujuana na kuwatambua watangazaji ambao wamekuwa wakiwabariki wasikilizaji wakiwa radio.

Tamasha hili lilihudhuriwa na maelfu ya watu, waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili zaidi ya 30, na wasikilizaji kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam. Katika tamasha hilo watoto walipata muda mzuri wa kufurahi kwa michezo mbalimbali iliyoandaliwa na kamati ya Mega Mkate na Praise Power.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ambaye ndiye mmiliki wa kituo hicho cha radio, aliwashukuru watu wote waliofika na wale ambao hawakufika kwa moyo wao wa upendo wa kusikiliza vipindi mbalimbali vinavyorushwa na radio hiyo. Pia aliwahubiria habari njema za Yesu, aliwaombea, aliwatamkia baraka na mwisho aliwaomba watu wazidi kuendelea kusikiliza radio hiyo ya dini kila wakati ili IMANI zao ziinuliwe na wawe karibu na Mungu kutokana na mafundisho yanayotolewa na watumishi wa Mungu mbalimbali. Kumbuka radio hiyo ni ya watu wote bila kujali dini, kabila, taifa, rangi, jinsia au umri.



































































































Comments