RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

08.04.2018: EMMANUEL MBASHA ALIVYMTUKUZA MUNGU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha alivyoweza kumtukuza Mungu na waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika ibada ya MAOMBI YA KUKOMESHA NJAA iliyofanyika siku ya Jumapili 08.04.2018. Watu walibarikiwa sana kwa uimbaji wake na watu waliitikia huduma yake kwa kishindo kikubwa. Uwepo wa Mungu ulitawala kupitia nyimbo zake zenye ujumbe mzuri wenye kufundisha, kauadibisha, kuelimisha na kukusogeza karibu na Mungu. Hakika Mungu ameweka kitu kwa mwimbaji huyu ambaye anatumia ujana wake kwaajili ya kumtangaza KRISTO kupitia huduma yake ya uimbaji. Tuzidi kumuombea ili Mungu azidi kuinua huduma yake na watu wapate kumjua huyu Yesu Kristo kupitia uimbaji wake. Unaweza kupata nyimbo zake mbalimbali kupitia youtube kwa Emmanuel Mbasha.

Tunakuliaka katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu akubariki sana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini Dar es Salaam.
Emmanuel Mbasha


















Comments