RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BLOGU YA MTUMISHI JAMES TEMU (UNCLE JIMMY) YATIMIZA MWAKA MMOJA

Siku ya jana ilikuwa ni siku ya pekee kwa mabloga na wapenzi wa kutembelea blogu za Kikristo Tanzania. James Temu (Uncle Jimmy) ambaye mbali na kuwa ni bloga pia ni mtangzaji wa radio ya Kikristo ya Praise Power ambayo iko chini ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God. Siku ya Ijumaa 19 Julai 2012 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa blogu yako, nikimaanisha ni siku ambayo blogu hii imetimza mwaka mmoja sasa.

Blogu ilivalishwa nepi na kunyweshwa maziwa ya mama. Wadau na mabloga walijiachia sana siku hiyo kwa kuonja utamu wa Yesu kutoka kwa waimbaji mbalimabali kama Bahati Bukuku, Flora Mbasha, The Empire na wengine wengi.

Kiukweli bloga wenu wa Ruma Africa, nilifurahi sana na juhudi na kazi nzima aliyoifanya James Temu. Nilibaki nashangaa mpaka nikasahau kupiga picha kwaajili ya kukutupia . ha ha ha ha ha!!!, lakini halijaharibika jambo kwani kulikuwa na mabloga wenzangu kama Victor na Papa waliokuwa wanafanya kazi ya Bwana kwa kuchukua matukio.

Nilifurahi kusikia hotuba ya Uncle Jimmya hasa pale alipowakumbuka na kuwashukuru watu walioshiriki kuiborsha blogu yake akiweo Rulea sanga ambaye amefanya urembo wote unaouona katika blogu yake.

Uncle Jimmy alikuwa na uhitaji wa vitu kadhaa kwaajili ya blogu yake, vitu hivyo ni kama Camera ya kisasa, Voice Recorder na alisema Mungu akipenda Pikipiki au bodaboda kwaajili ya kufika sehemu ambazo hazifikiki kwa gari. Jumla ya pesa ambazo zilikusanywa cash na ahadi ni Tsh. 1,500,000.

Unaweza kujiuliza ni blogu gani hii tunayoielezea kwako mdau wa Ruma Africa, blogu inaenda kwa jina la www.unclejimmytemu.blogspot.com

Sasa tupia macho yako hapo down uone kazi ya BWANA ilivyopendeza, watu wa MUNGU wanavyopendeza wakiwa katika mitoko kama hii:-


Uncle Jimmy (kushoto) akiteta jambo na Noel Tenga

"Jimmy umefanya kitu cha maana sana, kutukutanisha wapenzi wa blogu Tanzania........ Blogu yako kwa siku ya kwanza ilinifurahisha sana na sasa mimi ni mmoja wa wafuasi wako. Mimi kama mchungaji nitachangia Ths. 300,000", alisema Mchungaji Deo Lubala wa kanisa la WordAlive Sinza Mori
Rosemary kulia na mke wa MC Luvanda, wakitokelezea
 Ma Mc Wa Event Papaa Ze Blogger and Mc Pilipili

Fuluuuu furaha kwa wadau wa mablogu nchini Tanzania
 Pascal Itangaja kushoto na Kwa nyuma Ze Blogger Victor wa Hossanainc akiwa Kikazi Zaidi
 Dar-es-Salaam Band Wakienda Sawa Usiku Wa jana
  " Vipi mama nimetokelezea freshi lakini?"......Emmanuel and Florah Mbasha ndani ya Tamal Hotel
Kama bloga wenu, huyu dada namkubali sana kwa kazi zake anazofanya, hasa ukisiliza huu wimbo wake mpya, utamkubali....huyu si mwingine ni Bahati Bukuku a.k.a Big
 Pastor Deo Lubala (kushoto) ambaye alitoa mchango wake wa Tsh. 300,000.
"Tuko poa na Yesu wetu" ila hatuji wewe kama uko poa na huyo unayemwamini
"Jamni leo mnataka niimmbe wimbo gani?"...Bahati Bukuku akiwa kati na Ma-MC
 Wadau
 Mbona tulikoma hii Champagne kufunguliwa kwa manjonjo kama nusu saa hivi
  "Duh leo lazima tuonekane kwenye mablogu, si unajua hilo mke wangu?"...Mc Luvanda ambae ni CEO wa kampuni ya EDTONY akiwa na Mkewe Edna ndani ya Tamal
"Hamna kukimbia hapa Sama, nimekubana mpaka tuonekane kwenye mitandao!!'', "Poa mimi niko fresh".......Irony Lady Weda Ringo (kulia) na CEO wa Papaaz Entertainment Papaa Ze Blogger
 Mwendo wa Keki ulikuwepo
  "Utajuajeeeee, kuwa nayaweza mavituzi ya God??? Acha nikuonyeshe Jimmy."....Esta Wa Double E Sisters (kushoto) na Uncle Jimmy
"Nasema tuacheni tumsifu Mungu kwa raha zetu....tunakushukuru Jimmy mzee wa matukio....leo ni leo"
  "Bwana asifiwe, sisi ni kikundi cha The Empire....sio Vampire..hahahahah!! Jimy tunakupa big Up kwa kazi yako nzuri, mimi nimetembelea blogu yako kama mara mbili, na sasa ni member wako, nitawaeleza na jamaa zangu wawe ma-members"
 Kikundi cha IMUKA Singers ambao Kesho watakuwa Diamond Jubilee wakiwa ndani ya Tamal
Duh mbona huyu dada ananishinda kwa kunengua, nitajitahudi, sikubali kuaibika mbele ya wadau wangu wa blogu yangu....Hunishindi ng'ooooooooo!!!"....MC Papa akiwa na mwimbaji wa IMUKA Singers
 Kulia ni Bahati Bukuku, G katikati na Kushoto ni Dorcas Sakani
  "Mc Pilipili mbona unaongea sana, niache niongee"....Papa Sam

  Tuko Poaaaaaaaaaaaaaaa?
 The Empire wakiwa wametengeneza Empire
"Wewe acha tu, watu watajuaje"...Dada Jack.alinog

Comments