RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KWANINI NATESEKA WAKATI YESU YUKO?


Kama wanadamu kuna mengi tunapitia katika maisha yetu,na kuna changamoto nyingi tunazipata katika mahangaiko ya kutafuta maisha bora. Kuna wengine maisha bora walishawapata lakini maisha yao ni ya mateso sana, pesa au mali zao zimekuwa hazina msaada katika maisha yao. Mungu haangalii sana mali zako wala pesa yako kukupa furaha na amani katika maisha yako. Tumeona watu wengi wanaishi katika majumba ya kifahari sana lakini hawana amani ndani ya mioyo yao, wasiwasi umetawala. Watu wa namna hii hawatamani hata kulala katika majumba yao kutokana na mateso wanayopata. Wengine ni wagonjwa sana na wamejaribu kwenda katika mahospitali makubwa kutibiwa lakini imeshindikana. Pesa zao zimekuwa hazina msaada kabisa. Kuna wengine wamejariwa kuwa na vyakula vya kila naman lakini kutokana na magonjwa yao wameambiwa baadhi ya vyakula wasile na wakila watakufa. Wengine wana magari ya kifahari sana lakini hawayatumii kutokana na magonjwa walionayo, na magari hayo yanatumika na watu wengine kabisa ambao hawakutoa jasho la kuyatafuta. Ki ukweli maisha yamekuwa hayaeleki kabisa.

Wewe unapolia unaumwa kichwa, wapo wanaokatwa miguu huko mahospitalini, wewe unapolia unaumwa malaria wapo wanaoondolewa macho na wanakuwa vipofu, wewe unapolia kuumwa tumbo wapo wanaokatwa mikono na kuwa vilema. Kwahiyo kila mtu anakilio chake.

Ndugu wamekuwa hawapendani katika familia zao, utaona ndugu yako wa damu anaamua kukuchezea kwa kukutupia majini au magonjwa ya ajabu. wengine wanathubutu kwenda kwa waganga kukuharibia maisha yako, na hii inatokana na wivu wa mamendeleo yako. Mapepo yanaanza kukusumbua na kukuabisha kwa kukuangusha mbele za watu, amani inatoweka kabisa. Ndugu yangu unayefanya mambo hayo ipo siku yatakurudia na utaabika.

Mimi sio wewe na wewe sio mimi, shida zangu sio shida zako na shida zako sio zangu, kucheka kwangu kwaweza kuwa kero kwako, na kero zako zaweza kuwa kicheko kwangu, kwahiyo tunatofautiana.

La msingi katika haya yote ni kutua mzigo wako kwa Yesu, na ukifanya hivyo huku ukimaanisha, ndugu yangu utafurahia hayo majumba yako, magari yako ya kifahari, magonjwa yako yatatoweka, amani katika maisha yako itatapakaa kila mahali. Unaweza kujiuliza kuwa utatuaje mizigo yako kwa Yesu:
Kwanza mkubali Yesu kuwa kiongozi wako na hakuna mwingine zaidi yake.

Pili, fanya yale ambayo Yesu anataka uyafanye kwa uaminifu.

Tatu, Maagizo ya Yesu utayapata kwa kusoma Biblia na sio kusoma tu, bali kuyatendea kazi.

Nne, Shirikiana na wenzako katika kujadili yale ambayo umeyasoma katika Biblia ili imani yako iwe juu

Tano, Kuwa na imani ya kutosha kwa kuamni kila kitu kilichoko katika Biblia na yaamini maombi unayoomba

Sita, Uwe mtu wa maombi sana, hata kama unapitia katika magumu ya aina gani wewe kazana na maombi.

Kwa leo ngoja niishie hapo, Munguakinipa uhai tena tutazungumza mengine.

Asante Sana kwa kupoteza muda wako na kusoma kile Mungu amenielekeza nikifanye kwako.

Comments

Unknown said…
Mtumishi wa Mungu, ahsante sana kwa neno la leo, kwa kweli umelenga mahala pake. Huwa pia nashangaa ni jinsi gani binadamu ambao hapa duniani tunapita tu, tunakuwa na chuki na hatuna upendo baina yetu kwa ajili ya vitu vya duniani na vya kupita. Nakushukuru pia kwa kuelezea njia kuu sita za kuweza kutua mzigo unaotuelemea katika maisha yetu kwa Bwana Yesu. Ubarikiwe sana.