RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KILIO CHATANDA KATIKA IBADA YA KUMUENZI MWIMBAJI WA JOYOUS CELEBRATION WA AFRIKA KUSINI


Rumafrica inawapa pole sana wafiwa wote na pia wananchi wa Africa Kusini kwa kuondokewa na mpenzi wao na mpiganaji wa Yesu kuhakikisha dhambi zinateketezwa kwa njia ya uimbaji. Mungu amlaze mahali pema peponi na akumbuke kazi zake akiwa duniani...Amen

Marafiki wa marehemu na waimbaji wa zamani wa Joyous wakitoa faraja kwa uimbaji.©Phenyo

Hizi ni baadhi ya picha za baadhi ya waimbaji wa zamani wa Joyous Celebration na marafiki wa aliyekuwa mwimbaji wa kundi hilo mwanadada Thembililhe Berly Mbanjwa Sowazi aliyefariki dunia jumapili asubuhi kwa ajali ya gari nchini Afrika ya kusini wakati wa ibada ya kumuenzi na kumshukuru Mungu iliyofanyika huko Johannesburg.

Waimbaji walioacha gumzo katika ibada hiyo siku ya jana alhamisi ni Ntokozo Mbambo,Mahalia Buchanan,Brenda Mtambo,Hlengiwe Pitso,Duduzile Tsobane, Ntombizodwa Mahlangu pamoja na Kuki ambao wakiongozwa na Ntokozo waliimba wimbo 'Healer' wenye maneno mazito ya kufariji na yenye kuleta matumaini. wimbo huo aliimba Ntokozo akiwa na Joyous unapatikana katika DVD ya 15 part 2 ya kundi hilo.

Ukiachana na waimbaji hao pia ibada hiyo ilihudhuriwa mwimbaji Judith Sephuma, mama Sibongile Khumalo bila kusahau baadhi ya waimbaji wa Joyous Celebration ambao kwa pamoja waliweza kutoa faraja kwa wafiwa kupitia uimbaji wao, huku mwanadada Duduzile Tsobane akiwawakilisha marafiki zake katika kutoa salamu zao namna walivyoshirikiana na marehemu. Ibada ya mazishi ya mwimbaji huyo inatarajiwa kufanya jumamosi asubuhi katika kanisa la Grace Bible lililopo Pimville Soweto nchini humo.

Duduzile akiongea kwa niaba ya marafiki zake.

Mahalia,Hlengiwe,Kuki,Brenda,Ntokozo pamoja na Ntombizodwa wakimsikiliza Dudu akizungumza kwa niaba yao, hayupo pichani.

Ntokozo akiongoza wimbo Healer, huku Dudu na Zodwa wakisubiri kuitikia.

Healer ikiimbwa kwa hisia

Mambo ya uimbaji yananoga sana kama waimbaji mnajuana uwezo wenu wa kuimba

Nyota wa zamani wa Joyous wakitoa faraja na wimbo 'Healer'.

Marehemu Lihle Mbanjwa Sowazi siku ya ndoa yake.

Marehemu Lihle siku ya harusi yake mwishoni mwa mwaka jana, inaelezwa hili gauni lilikuwa ndoto yake siku akiolewa, ikatokea hivyo.©Hlengiwe, Phenyo na Sylvester.

wimbo wa "Healer"

Thanks
Gospel Kitaa

Comments