RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA YASHANGAZWA NA NGUVU ZA MUNGU KWA KUPITIA NABII FLORA PETER SIKU YA JUMAPILI 02.12.2012 BAADA YA KUANGALIA DVD ZA HUYO NABII FLORA

IBADA ILIYOONGOZANA NA UPAKO WA MAFUTA

Jumapili ilikuwa ni Jumapili ya pekee katika kanisa la Huduma ya Maombezi ya Nabii Flora Peter, watu walipokea miujiza yao baada na kabla ya kupakwa mafuta yenye upako wa ajabu. Watu wengine walilete hilizi zao za uchawi ili zichomwe moto na kumpokee Bwana Yesu Kristo. Nabii aliwaambia waumini wake ya kuwa hataki kuona watu wanakuja kuabudu huku wamebeba hilisi zao kwani kanisani ni sehemu ya Mungu, na kama umekuja nazo iwe ni  kwajili ya kuzichoma na sio urudi nazo nyumbani.

Pia alisema ameguswa sana na wimbo wa mwimbaji wa nyimbo za injili Stella Joel kwa wimbo wake wa HAKUNA MMANAMKE MBAYA alioimba katika ibada ya jumapili hii. Nabii Flora alihubiri Neno la Mungu kwa waumini waliofika katika ibada hiyo ya Jumapili, na haya ndiyo aliyonena madhabahuni:-

Nabii Flora Peter akimwimbia Mungu kabla ya maombezi kuanza


MAOMBI
Maombi yaliyofanyika kabla ya zoezi la kupakwa mafuta kuanza, na haya ndiyo aliyoyaomba, Nabii Flora Peter:

Bwana Yesu asifiwe wapendwa wa Mungu…..Mpendwa naomba siku ya leo utulie katika kiti chako upate kuokolewa siku ya leo. Tutaanza maombi ya deliverance, lazima ufunguliwe siku ya leo. Nimeapa siku ya leo kuwa kila mwenye mateso, ninaenda kuyavunja vipande vipande. Nimeapa maisha yako lazima yabadilike, una kesi mahakama lazima ushinde kwa kupakwa mafuta haya ya upako. Tuko hapa kwaajili ya kutangaza jina la Yesu, tunataka watu wamuone Mungu wao.  Wapendwa leteni watu kwa Yesu waokolewe.

Ninaachilia neema kwa wasio zaa, na watapokea ujauzito kwa kupakwa mafuta, nyumba zako zilizonyang’anywa lazima zirudi kwa jina la Yesu. Amini Mungu anaenda kufanya haya kwako siku ya leo.

Unaweza kuwa na mume wako na akaweza kukugeuka, lakini ni Yesu peke yake ni rafiki mwema. Hata mchumba anaweza kukukimbia lakini Yesu hawezi kubadilika, ni Yeye yule. Yesu ni rafiki wa kweli. Na tazama ninaona wingu limetanda mahali hapa, nainaona nguvu ya Mungu, ninaona malaika wamekaa wakisubiri kushuka kutenda kazi pamoja na mimi. Kuna watu wamekusudiwa na Mungu kutendewa mema siku ya leo. Ni siku chache kumaliza mwaka na huu mwezi wa Januari ni mwezi wa kurejesha biashara yako, mali zako zilizotekwa zinaenda kurejeshwa




Nabii Flora akiomba


MAOMBI WAKATI WATU WAKIPAKWA MAFUTA
Nabii Flora alikuwa akiwaombea watu huku akiwapaka mafuta katika uso za waumini wake huku akitamka baraka huku wamumini wakiwa wamenyoosha mikono yao juu kama ishara ya kusalenda kwa Yesu, naye Nabii Flora alikuwa na haya kusema:

Kwa damu ya Yesu na upako huu wa mafuta Bwana anaenda kunyoosha maisha yako..kwa imani pokeea kwa jina la Yesu. Wale waliokufa kwa njia za kulogwa wataenda kufufuka kwa jina la YesuBwana aende akatendee miujiza katika nyumba yako mpendwa. Pokea uzima ewe mama ewe baba kwa jina la Yesu. Natangaza mlipuko usio wa kawaida maana umesema hizi ni siku za mwisho, na ninamomba watu hawa kufute magonjwa siku ya leo, ukafute misiba kwa jina la Yesu, waliovunjikam mioyo wakainuliwe, wenye biashara zikafanikiwe. Baba leo ni siku tukufu na ni mwezi hatari wa Mungu, mwezi wa kurudisha vilivyopotea. Tunasambaratisha magonjwa na mikosi kwa watoto wadogo wanaopakwa mafuta haya. Mungu onekana kwa wale waliokata tama. Baba angalia ibada ya leo, siku ya leo ikawawe ya tofauti, kaangalie watumishi wako, anagalia wale wanaofanya kazi ya Mungu katika kanisa hili.

Watu wa Mungu siku ya leo narejesha uchumi wako ulioyumba, kama huna mume/mke naenda kuonyesha siku ya leo, ninaenda kutoa mikosi siku ya leo.

Ee baba tembelea watu wako, huu ni wakati wa matendo makuu ya Mungu, ninasema kila sehemu nguvu ya Bwana ifike kwa jina la Yesu, Baba tunahitaji nguvu yako itembee pande zote, watu warejeshewe mali zao, warejeshewe watoto wao. Watu hawa wapate mafanikio. Bwana achilia neema yako, Bwana tembelea kanisa lako sasa.

Wewe pepo ulikula maisha ya watu hawa nakuamuru uachie baraka za watu hawa kwa jina la Yesu. Watu uliowapotesa wewe shetani unaenda kurudisha kwa jina la Yesu.

Mimi nimetumwa kutangaza habari njema na matendo makuu ya Mungu, nakuambia leo unaenda kupokea Baraka. Naona sanduku la baraka, sanduku la uponyaji linakuja kwako mtu wa Mungu, Yesu anakuja kukubariki leo mtu wa Mungu, naomba uamini sasa, imani yako inaenda kukuponya kwa jina la Yesu.

Ninageuza hewa mahali hapa, nageuza manukato katika kanisa hili kwa jina la Yesu, hewa kutoka kwa mungu na manukato ya Mungu yanakujia sasa..Pokeeeea kwa jina la Yesu. Utukufu wa Mungu unazidi kushuka sasa, naona wewe unayeumwa kifua unaponywa sasa, na wewe unayenitazama iko neema kwako, pokea hiyo neema katika maisha yako

Yesu alisema waache watoto wadogo wangu waje kwangu, sasa Yesu naomba utembelee watoto wako



UTAMBULISHO WA STELLA JOEL
Stella Joel ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania ambaye anatokea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B. siku ya jumapili aliaaliwa na Nabii Flora Peter katika huduma ya uimbaji katika kanisa la Huduma ya Maombezi Mbezi Salasala

Kutoka kulia ni Nabii Flora Peter, Mwimbaji wa nyimbo za injili Stella Joel akitambulishwa kanisani kabla hajakaribishwa kuimba madhabahuni

Nabii Flora na Stella joel katika picha ya pamoja

Stella Joel akifurahia uimbaji wa Praise Team

Stella Joel akiimba wimbo wa Hakuna Mwanamke Mbaya ambao uko katika albam yake mpya iliyobeba wimbo huo

Kushoto ni Bukuku akiwa na Nabii Flora na stella Joel katika picha ya pamoja


UJUMBE WA LEO
Tusome Kutoka 15:20, Ndipo Musa na wana wa Israel wakamwimbia Bwana wimbo, wakamwimbia Bwana wimbo huu na wakanena na kusema, nitamwimbia Bwana kwakuwa ametukuka sana. Tazama farasi na wapanda farasi bwana amewatupa mbali, Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu naye amekuwa wokovu wangu, yeye ni Mungu wangu nami nitamsifu, ni Mungu wa Baba yangu nami nitamtukuza. Bwana ni mtu wa vita. Na Bwana ndiye jina lake, magari ya farao na majeshi yake ameyatupa baharini, na maakida wa wateule wamezama katika bahari ya Sham, vilindi vimedumbukizwa. Mkono wako wa kuume umewasetaseta maadui zako. Nguvu ya  mkono wako wawaangusha chini wanaopotea
 Nabii Flora akiomba, kutabili na kukemea mapepo
Mwezi wa kumi na mbili ni mwezi ya kurudisha nara. Tumebahatika kuingia mwezi huu, tutamshangilia Mungu wetu. Bwana wetu ni mtu wa vita, kwa mwezi huu atapigana na maadui zetu. Kama nabii wako nitarudisha watoto wako, nitarudisha mafanikio yako, nitarudisha kibali chako, naachilia kibali cha Bwana. Maana Bwana ni mtu wa vita, maadui zako waliokufatilia lakini kwa kuingia mwezi wa kumi na mbili, majeshi yao magari yao yametupwa baharini, waleokurudisha nyuma wameshindwa wanaenda kukuachia na utasonga mbele.

Watu hawa hawapendi kuangushwa na mapepo lakini nguvu ya Mungu ndiyo inafanya hivi kuwakomboa katika kifungu ha shetani.

Maadui zako wamezama katika bahari, mateso yamezama, lazima UKIMWI uzame, lazima magonjwa yazame, lazima kansa izame, Yesu ameleta njia ya kweli. Nyoosha mkono wako na useme maadui zako wamesetwasetwa kwa mono wangu huu wa kuume na kila kilichopotea kinaenda kupatika kwa jina la Yesu. Yesu ataenda kuwaangusha chini adui zako Mkono wa Bwana upo mahali hapa kuangamiza maadui zako, magonjwa yako, kansa, UKIMWI, Umaskini, mateso. Madui zako watazamishwa mahali hapa,

 Waumni wakifuatilia maombezi
Ni nani aliye kama Mungu kwa utukufu wake?  Kwa kutumia nguvu za Mungu ninapandisha biashara za watu, hii nguvu itembee kwa watu walioko kwenye miti wananitazama na kunisikiliza. Tazama Bwana kwa rehema zako wewe unawakomboa watu wenye mateso, kwa uweza wako Bwana unawaelekeza watu, Nami nabii naona moto wa Mungu unashuka kwako, pokea baraka zako sasa mtu wa Mungu. Pokea damu ya Yesu Kristo.
 
Mapepo yakiwatoka wakati wa maombezi
Kabila za watu wamesikia matendo makuu ya Mungu na sasa wanatetemeka, watu waliosikia habari zako sasa waliokufa wanafufuka, watu wanashangaaa kuwa hiki ni kitu gani anafanya nabii Flora kutoka na uwepo wako Mungu. Huu ni wakati wa manabii kutenda, na ni wakati wako huu wa kupokea.

Watu wanasikia habari zako Mungu wanateteleka na maadui wanahangaika, lakini wewe unayesikia habari hizi za Mungu unaenda kubarikiwa, kama nabii wa Mungu narejesha mafanikio yako, vitu vyote ulivyopoteza tunarejesha.
Mapepo yakikimbia kwa jina la Yesu
Watu wenye nguvu na mafedha yao leo wanaenda kutetemeshwa na nguvu za Mungu, mali zao hazifanyi kazi ya Mungu bali kuwatesa watu wa Mungu, leo ni siku yao. Naachilia tetemeko kwa madaui zako, wale waliochukua furaha yako, waliokudharau nawatetemesha. Na mwaga damu ya Yesu katika kanisa hili ikikumwagikie


Maadau zako wamerushwa na hofu imewaajilia na watakaa kimia siku ya leo. Mwaka 2013 tunaenda kuvuka kwa kishindo kikubwa kama watoto wa Mungu na maadui zako watanyamaza kimia, magonjwa yatatoweka. Tutaingizwa na kupandwa katika mlima wa uridhi wa Mungu. Hautakufa lazima uvuke na kufikia 2013. naomba uiname na kugusa chini huku ukisema nimepanda katika urith wa Mungu.

Kama nabii ninakuambia hautakufa kwa ugonjwa, hautakufa kwa stroke kwani Bwana amekupanda siku ya leo. Bwana anasema nimewaweka katika patakatifu pangu na nitawatawala milele na milele na hakuna mtu atakayekanayaga shamba lako tena, Bwana atakupandisha mtu wa Mungu

BAADA YA MAOMBEZI

Wale wote waliokuwa wanahitaji baraka zao zipande waliambiwa wapeleke maji kwaajili ya kuombewa


 Mzee wa kanisa kulia akimsikiliza nabii Flora kwa umakini sana
 Mtafsiri wa kanisa akiwa ameshika hilizi kutoka kwa mmumini tayari kwa kuchomwa moto.
 Mchungaji Jury akisema jambo madhabahuni

Mchungaji Jury akiomba







 Kulia ni Leah ambaye ni mwimbaji wa hapo kanisani na ni Mwalimu wa shule ya Msingi hapa jijini Dar es Salaa






SHUHUDA
MAMA APATA UCHUNGU WA KUZAA WAKATI WA MAOMBEZI

Mama aliyepata uchungu wakati wa maombezi, na Nabii Flora wakati ibada ikiendelea alimpa fedha kwaajili ya kwenda hospitalini kujifungua
ANGALIA SHUHUDA ZINGINE KWA
KUBOFYA HAPO CHINI "Read More"


(Rumafrica inakuoma radhi kutokuletea shuhuda za hawa wapendwa, bado ninaziandaa)






















Comments