TB JOSHUA IMAGES WI MSG

AFRICAN CRYING

AFRICAN CRYING

RUMAFRICA CONTACTS

Tuesday, October 6, 2015

KANISA LA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES LAFANYA MAOMBEZI NA KUKEMEA NDOTO MBAYA

Jamani kuna watu wana kiu ya kumuona Mungu akifanya mambo makuu katika maisha yao. Hii ilionekana katika Ibada Takatifu iliyofanyika katika  kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God lilipo Mikocheni "B" Dar es Salaam Tanzani kwa Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatarea, watu waliweza kufanya wawezavyo kwa kutaka kumugusa Mungu wetu kwa njia ya maombi.
Katika ibada zozote tunaamini kwamba kila mtu anaingia ibadani akiwa na hitaji lake muhimu ambalo anataka Mungu wetu wa Mbinguni ametendee.
Hii ilijitokeza katika kanisa hili la Mungu baada ya askofu wa wakanisa hilo Mh. Dkt Gertrude Rwakatare alipomaliza kuwaombea, aliwaomba waumini wa kanisa hilo kuomba kile wanachotaka Mungu awafanyie. Kanisa lilijawa na kelele za maombi ambapo kila mtu aliweza kuomba kile anachotaka Mungu amsaidie.
Kama Wakristo tunaamini katika maombi kuna nguvu za ajabu sana, na kuna mambo mengi sana yanaweza kutookea baada ya kufanya maombi.
Kitu cha kuzingatia katika maombi ni kuiandaa imani yako iamini kuwa huyu ninayemuomba yupo hata kama kwa macho haonekani, ila kwa ulimwengu wa Rohoni anapatikana. 
Unatakiwa kujitakasa mbele za Mungu kabla hujaanza maombi yako binafsi ufanyiwe na Bwana, ikiwezekana tafuta mahali patulivu ili unaomba kusiwe na mwingiliano wa mawazo mengine wakati ukiomba, baada ya kumaliza kuomba jenga imani yako kuwa jambo lako Mungu kisha lifanya juu yako, usiwe mtu wa kulalamika unapoona hitaji lako halijafikia kwa wakati.
Kila mtu anatambua kuwa Mungu wetu hana upendelea, ni Mungu wa haki kwa kila mmoja, kwahiyo unapoomba na wenzako utambue ya kuwa Mungu atawapa wote. Tuombe sana Mungu maombi yetu yasiwe ya mashindano, bali wewe omba ukimwangalia Mungu tu.
Kuna mengi tuweza kuongea na wewe, lakini unaombwa sana kutembelea blogu yetu ya www.mountainoftanzania.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot. com

 
BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KUONA MWENDELEZO WA MATUKIO HAYA

KIFO CHA MTIKILA; BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LAAHIRISHA KIKAOKutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa nchini, Peter Kuga Mziray, Msajili Msaidizi vyama vya Siasa, Sist Nyahoza, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Monica Laurent.
Mwenyekiti Baraza la Kamati ya Bunge na Siasa na rais wa TADEA , John Lifachipaka (kushoto), Peter Kuga Mziray (akisoma taarifa yake), Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa na Sist Nyahoza.
Wanahabari wakichukua tukio.

Isome habari yote hapa===>PRESS MSIBA OCT 20150001

NA DENIS MTIMA/ GPL

TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA


Christopher-Mtikila

Marehemu Christopher Mtikila enzi za uhai wake.
Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.
Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.
Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.
Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.
Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.
Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.
Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:
  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim

MASWALI 10 TATA KIFO CHA MTIKILA!

Na Waandishi Wetu
BASI tena! Kifo cha ajali ya gari cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP) na Kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, Mchungaji Christopher Mtikila kimewaacha wananchi na majonzi makubwa lakini nyuma yake, Uwazi limebaini maswali 10 tata kuhusu ajali hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP) na Kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, Mchungaji Christopher Mtikila enzi za uhai wake.

Ajali hiyo ilitokea saa kumi na mbili asubuhi ya Jumapili iliyopita, eneo la Msolwa, Chalinze wilayani Bagamoyo, Pwani ambapo gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 189 AGM lilipoteza mwelekeo na kuingia bondeni. Mtikila alipoteza maisha papohapo huku watu watatu, akiwemo dereva wa gari hilo wakinusurika.

WALIOKUWEMO
Mbali na Mtikila watu hao watatu ni dereva George Ponela, Ali Mohamed (msaidizi wa dereva) na Mchungaji Patrick Mgaya ambaye anatajwa kuwa msaidizi wa marehemu Mtikila.Hata hivyo, baadhi ya watu waliozungumza na Gazeti la Uwazi juzi, nje ya Hosptali Teule ya Rufaa Mkoa wa Pwani, Tumbi walionesha kuwa na maswali kumi yenye utata juu ya ajali hiyo na kifo cha Mtikila.

SWALI LA KWANZA
Swali la kwanza lenye utata ni gari hilo kufika bondeni kwa kubiringika lakini mwonekano wake hautoi picha kwamba limebondeka kutokana na kulala na kuinuka mpaka lilipofika mwisho.


Mchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa na aliyekuwa na marehemu wakati wa ajali
.

“Unajua kwa kawaida, gari likibiringika kutoka juu kwenda chini lazima litabondekabondeka. Nadhani mliona lile gari la yule msanii marehemu Sharo Milionea (aliyepata ajali, Muheza,Tanga). Pia mliona gari la marehemu Chacha Wangwe (aliyepata ajali Kongwa, Dodoma),” alisema mkazi mmoja Kibaha, Pwani.

SWALI LA PILI
Akaendelea: “Mimi nimeona picha ya marehemu halafu nimesikia maelezo ya mmoja wa waliokuwemo, eti marehemu alilaliwa na gari. Hivi mwili unaolaliwa na gari unakuwa vile jamani? Labda lakini, mimi si mtaalam sana wa miili ya ajali. Lakini naamini angekuwa na majeraha ya kukandamizwa.”

SWALI LA TATU
Naye muuguzi mmoja wa Hospitali ya Tumbi alishangazwa na dereva ambaye anashikiliwa na polisi na msaidizi wake kutoka salama kwenye ajali hiyo ya gari kubiringika.“Watu wengine sijui ni bahati au nini? Gari libiringike vile halafu utoke salama, inawezekana kweli? Au kwa sababu kila mtu ana siku yake ya kufa aliyopangiwa na Mungu,” alisema muuguzi huyo.

SWALI LA NNE
Uwazi lilizungumza na Mchungaji Mgaya, nje ya hospitali hiyo. Yeye kaumia kidogo kwenye paji la uso.
Kwa upande wake alisema: “Gari lililopata ajali lilikuwa la kukodi. Mtikila alikodi kutoka Dar kwenda Njombe na kurudi Dar. Wakati wa kurudi ndiyo tukapata ajali.”Lakini chanzo kingine cha jijini Dar kilipozungumza na Uwazi na kutajiwa aina ya gari, kilisema: “Hilo gari litakuwa la Mchungaj Patrick Mgaya.”

SWALI LA TANO
Mtu mmoja aliyejitaja kwa jina la Mike, alizungumza na Uwazi nje ya Ofisi za Global Publishers juzi mchana na kusema kuwa, Jumamosi usiku alimpigia simu Mtikila kwa mazungumzo yao, Mtikila akasema yupo Dar.
“Sasa kusikia eti kafariki dunia akitokea Njombe nimeshangaa sana. Kwa nini aliniambia yupo Dar wakati mimi si adui yake wa kunikwepesha ukweli?” alihoji Mike.


Ali Mohamed miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo.

SWALI LA SITA

Kwa mujibu wa Mchungaji Patrick, wakati wanarudi, dereva wa gari hilo alikuwa akienda mwendo wa kasi mpaka Mtikila akawa na kazi ya kumwambia mara kwa mara, ‘we bwana mdogo punguza mwendo, utaleta matatizo bwana.’ Alikuwa akipunguza kisha anaongeza tena na Mtikila naye alikuwa akirudia tena kumsema.
Swali hapa ni kwa nini dereva alikuwa akipenda kuongeza mwendo licha ya kutahadharishwa? Kama Mtikila alikodi gari hilo si ndiye alikuwa bosi! Kwa nini dereva alikuwa hataki kumsikiliza bosi wake?


SWALI LA SABA
Eneo la Msolwa lina watu au wanakijiji. Mara nyingi inapotokea ajali, wanakijiji hujitokeza kwa wingi kushuhudia. Kwa nini wanakijiji wa Msolwa hawakujitokeza? Picha za eneo la ajali hakuna inayomwonesha mwanakijiji hata mmoja.

SWALI LA NANE
Namba za gari kuwa A (AGM) linazua maswali kwamba ni kweli lilikuwa na uwezo wa kutoka Dar hadi Njombe na kurudi Dar? Kwa tarakimu za sasa za magari ni D. Kwa hiyo A ni magari ya muda mrefu, 2007.

SWALI LA TISA
Mwili wa Mtikila ulikutwa umelala, shati alilovaa siku hiyo ni jeupe! Kama gari lilibiringikia bondeni, kwa nini shati lisichafuke?

SWALI LA KUMI
Pia wananchi walioona picha za mwili wa Mtikila wanahoji kwa nini mwili usiwe na majeraha, mchanga au vumbi?

KWA MUJIBU WA MCHUNGAJI MGAYA

Akizungumzia ajali hiyo kwa undani, Mchungaji Patrick Mgaya alisema:

“Tulikuwa tukitoka Njombe katika mkutano wa kisiasa. Tulipofika Msolwa, Pwani leo (juzi) alfajiri kama saa 11:45 tukiwa katika gari dogo tukapata ajali mbaya sana iliyosababishia kifo cha Mtikila, nasi tukawa tumepata majeraha.
“Ninachokijua ni kwamba, dereva wetu, George Ponela ambaye tulipewa katika gari hilo tulilolikodi alikuwa akiendesha kwa mwendo mkali hadi spidi mita 140 tukawa tunamkataza.
“Marehemu alikuwa akimkataza mara kwa mara, akawa anapunguza mwendo wakati fulani lakini akawa anarudia katika hali hiyo ya kuongeza.”ILIVYOKUWA “Marehemu aliona ni jambo la hatari kwani linaweza kusababisha mauti lakini dereva hakumsikiliza. Tulipofika Msolwa, tukaona lori limesimama mbele yetu, dereva wetu akawa analipita. Ghafla akaona lori lingine mbele yake, ikabidi atoke nje ya barabara.

“Kusema kweli ile ajali nilishaiona kwa macho. Nikaamua kushika kiti cha marehemu na cha dereva maana nilikaa siti ya nyuma na msaidizi wa dereva. Wakati gari linapinduka, wenzangu wote walirushwa nje.
“Baada ya gari kutulia, nilitoka nje nikawaona wenzangu wakimtafuta Mtikila. Baadaye tulimwona chini ya gari, amelaliwa.”

NENO LA MWISHO LA MTIKILA
“Tulishirikiana kumtoa. Tulimkuta hajakata roho. Nikamuita mchungaji… mchungaji…mchungaji Mtikila. Neno aliloniambia la mwisho ni ‘BASI’. Akakata roho. Taarifa ikatolewa polisi tukachukuliwa na kuletwa hapa Tumbi.”

KUHUSU DEREVA
“Dereva anashikiliwa na polisi lakini sisi wawili tunapata matibabu hapa na Mtikila ndo’ hivyo katuacha na yupo mochwari. Kwa kweli mwendo kasi ulichangia na sijui ni kwa nini yule dereva alikuwa akikaidi amri ya Mtikila wakati gari lile lilikodishwa na yeye ni dereva tu siyo mwenye gari.”

Habari imeandaliwa na Makongoro Oging’, Issa Mnally na Haruni Sanchawa.

GWAJIMA APEWA SIKU 14 KUMFUFUA KAKA YAKE AU KUPANDISHWA KIZIMBANI

Shamma Gwajima (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kushoto ni Raphah Gwajima.

Watoto hao wakisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa waandishi wa habari kabla ya kuyajibu.

Wanahabari wakiuliza maswali.

Shamma akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ametumiwa waraka mzito na wanaodai kuwa watoto wa kaka yake Gwajima, Faustine Mathias Gwajima, ambaye kwa sasa ni marehemu, wakimtaka askofu huyo kumfufua baba yao ndani ya siku 14 la sivyo watamfikisha mahakamani kwa kile walichokitaja kuwa amewasababishia athari kubwa za kisaikolojia kwa muda mrefu.

Wakizungumza mapema leo hii na waandishi wa habari Idara ya Habari Maelezo, Jijini Dar, watoto hao waliojitambulisha kwa majina ya Shamma Gwajima (18) na Raphah Gwajima (17) walisema kuwa baba yao ambaye ni kaka wa Askofu Gwajima alifariki dunia mwaka 2008 mkoani Mwanza kwa maradhi ambapo Askofu Gwajima wanayemwita baba mdogo alifika msibani hapo na kuwataka ndugu na marafiki waliokuwa wakiomboleza kifo cha mpendwa wao wasihuzunike kwa kuwa marehemu hakuwa amekufa bali amelala tu.

“Mchungaji Gwajima alitukataza tusilie na tusihofu kwa chochote kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kumuombea marehemu hadi afufuke. Kauli hiyo ilitufanya tuanze kufurahi na akaushika mwili wa marehemu katikati ya umati wa watu na kuanza kuutikisa akimtaka baba yetu aamke lakini hakuamka,” alisema Shamma.

Watoto hao walidai kuwa tangu siku hiyo Gwajima aliondoka kimyakimya na kuingia mitini na kudai kuwa jambo hilo limewaathiri kihisia na kisaikolojia na wanajiandaa kumshtaki kutokana na usumbufu aliowasababishia katika kipindi kigumu cha msiba wa baba yao.

Watoto hao walienda mbali zaidi na kudai kuwa waliamua kukaa kimya wakiamini Askofu Gwajima ambaye ni baba yao mdogo anastahili heshima ya kichungaji mbele za watu, lakini walidai kuwa wanashangazwa na mambo ayafanyayo hivi karibuni kama vile kuwatukana watumishi wenzake na kutoa siri za waumini wanaoenda kwake kwa ajili ya kupata huduma za maombezi.

Aidha walidai kuwa Askofu Gwajima ni tapeli kwa kuwa anatumia huduma ya kufufua misukule ‘hewa’ kwa maslahi yake binafsi na kuitaka serikali iingilie kati kumchukulia hatua huku wakiitaka jamii isikubali udanganyifu wa askofu huyo kwa kuwa kama kweli anafufua watu basi angemfufua kaka yake.

“Je, misukule ambayo anatangaza ameifufua, tujiulize kabla ya kufariki ilikuwa ikiishi wapi? Na, je, kuna vyeti vya kifo vinavyothibitisha kama watu hao wanaofufuliwa walikufa kweli? Je, ndugu wa hiyo misukule wapo?” walisema watoto hao na kuongeza kuwa kutokana na kushindwa kwake kumfufua baba yao, Gwajima amewatelekeza kwa kutowapa msaada wowote licha ya yeye kuishi maisha ya kifahari.

(Picha/GPL/Chande Abdallah)

KUTOKA RUMAFRICA Online MAGAZINE..JIPATIE NEWS