RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO NKONE AACHILIA ROHO YA UIMBAJI KWA WAUMINI NAIOTH

Kila siku ina Neema yake hapa ulimwenguni, na ndivyo ilivyodhihirika Jumapili iliyopita wakati Mama Mchungaji Mbeyela, maarufu kwa jina la Upendo Nkone, muimbaji anayeinua mioyo ya wengo kwa nyimbo zake za kusifu na kuabudu.

Waumini kwenye kanisa la Naioth Gospel Assembly linaloongozwa na Askofu David Mwasota walipata nafasi ya kuinuliwa kwa huduma zao za uimbaji, hasa kwa wale ambao wana wito huo, pasi kujua waanze vipi na wapi.

Mwanamama Upendo Nkone alifanyika baraka siku hiyo, kwani alianza mkwa kuwaita madhabahuni wale wote wanojisikia kuwa na huduma ya uimbaji lakini wanasitasita, na wengine ambao walikuwa waimbaji lakini mambo yao hayaeleweki, na kisha baada ya hapo kuachilia Roho ya uimbaji kwa wote ili wapate kulitukuza jina la Yesu pasipo mashaka yoyote, zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo.


Askofu John Mbeyela na mke wake, Upendo

Kwa kweli Upendo umewazunguka watumishi hawa



Upendo Nkone akiwa na wale wote walioshiriki naye wakati wa shooting ya video album yake mpya

Kundi la wanaotamani kuimba na wale waliokata tamaa wasijue wapi pa kuanzia wakisifu Jukwaani na Upendo Nkone.

Kanisa zima likajawa na sifa

Mahubiri yakafuatia, mchungaji Rahel Mwasota akihudumu siku hiyo.

Thanks: GK

Comments