RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ERIC SHIGONGO AKIFUNDISHA UJASIRIAMALI NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES OF GOD KWA ASKOFU MH. GERTRUDE RWAKATARE

Eric Shigongo akiongea kwa huruma na hisia kali juu ya maisha yake ya taabu aliyopitia na hasa wazazi wake walivyodharauliwa na kutengwa na jamii eti hawana pesa. Baadhi ya waumini wa kanisa la Mlima wa Moto waliokuwa wakimsikiliza walikuwa wakitokwa na machozi.

Eric Shigongo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers iliyoko Dar es Salaam. Mfanyabiashara huyu anatoka katika familia maskini sana na ya kutupwa iliyoko Mwanza Tanzania. Alitokea kuchukia sana umaskini tangia akiwa mdogo sana. Mbali na kupata mafaniko makubwa sana kwa jitihada zake za kujituma katika kazi, ni mtu ambaye hajasoma na elimu yake ni darasa la saba. Umaarufu kwake umetokana na stori alizokuwa akiziandika katika magazeti.

Mungu amempa neema ya ubunifu na uchapakazi wake, na hivi vilimsaidia sana kutambua kuwa elimu sio suluhisho la mafanikio bali kazi yenye majtunda mazuri ndio kiini cha mafanikio. Pia ni mtum mbunifu na msumbufu wa kutaka kujua watu wanawezaje kufanikwa na kuwa matajiri. Eric Shigongo akikiri mbele ya Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare jinsi alivyosumbuana na mlinzi wa geti la Askofu kutaka kuingia kuonana na Akofu, anasema ilikuwa kazi sana kumuona lakini alijaribu kumsumbua mlinzi na hatimaye alifanikiwa na kuweza kuonana naye akiwa na lengo moja tu la kutaka kujua historia ya Askofu Mh. Gertrude Rwakatare ili iweze kumsaidia katika maiasha yake.

Katika kitabu chake kipya amejaribu kuelezea ni jinsi gani faida ya usumbufu inaweza kukusaidia kutimiza ndoto ya hapo baadae. leo hii Eric Shigongo ni mmoja wa matajiri wakubwa nchini Tanzania na utajiri wake unatokana na ubunifu na adabu katika kazi.

Sasa ukitaka kujua aliyoasema Eric Shigongo basi ingia Youtube, Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania. www.mountainoffire Tanzania
 Erid Shig
 





















Comments