RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA Online MAGAZINE1















































MWISHO

KIKAO CHA USHINDI CHAFANYIKA KATIKA OFISI YA RUMAFRICA
Kikundi cha kusaidiana cha ambacho kimewakusanya waimbaji wa nyimbo za Injili, wajasiriamali, wafanyakazi, na watu mbalimbali kiliweza kukutana katika ofisi za Rumafrica na kuweza kujadili maswala mbalimbali ikiwa pamoja na kutafuta jina la kikundi hicho na jinsi gani kikundi hicho kitaongozwa.

Kutoka kulia, Mwenyekiti Rulea Sanga,Uhamasishaji Enoce, Katibu Leah Mwankundile, Maombi Emmanuel Dobogo

Kikao kilifunguliwa kwa maombi yakiongozwa na mtumishi wa Mungu, Egid Chang'a na baadae kikao kiliendelea kama kilivyopangwa. Walioweza kufika siku hiyo ya tarehe 09/03/2015 ni Rulea Sanga, Egid Chang'a, Emmanuel Dobogo, Tumaini Njole, Enoce na Leah Mwankundile.

Kikao hicho kiliweza kupata jina la kikundi na kuitwa USHINDI na kabla ya jina hilo kilikuwa kinaitwa Rumafrica. Baada ya kupata jina hilo la kikundi, uchanguzi wa viongozi wa muda ulifanyika na ikaonekana Rulea Sanga kuwa Mwenyekiti, Tumaini Njole kuwa Mhasibu, Leah Mwankundile kuwa Katibu, Egid Chang'a kuwa kiongozi wa nidhamu na Enoce kuwa kiongozi wa kuhamasisha maswala yanayotakiwa kufanyika katika kikundi hiki.

Kikundi kimetokana na mtandao wa Watsap ambapo watu waliweza kufamiana kwa njia ya kutumiana ujumbe na baadae wakaona kuna umuhimu wa kufamiana zaidi na kuweza kusaidiana kwa mambo mbalimbali badala ya kuwa watu wa kuchart tu.

Kwa sasa kikundi hiki kimefikia hatua kubwa sana na kiko katika harakati za kwenda hatu nyingine kubwa kwaajili ya kusaidiana na hapo baadae kinategemea kuifikia jamii yenye uhitaji na kusaidiana. Kama ungependa kujiunga unaweza kuwasaliana na Katibu wa Chama hiki Leah Mwankundile  kwa simu +255 656 219 865.
 Kutoka kulia ni Katibu Leah Mwankundile, Kiongozi wa Nidhamu Egid Chang'a, Kiongozi wa Uhamasishaji Enoce, Kiongozi wa Maombi Emmanuel Dobogo
 Tumaini Njole (kushoto)

  Kutoka kulia ni Katibu Leah Mwankundile, Kiongozi wa Nidhamu Egid Chang'a, Kiongozi wa Uhamasishaji Enoce, Kiongozi wa Maombi Emmanuel Dobogo na Muhasibu Tumaini Njole