RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA Online MAGAZINE-CLICK BELOW





















































































































































































































































 























































































































































































 





































































































































































































































































































\
























































































































































MWISHO

KIKAO CHA USHINDI CHAFANYIKA KATIKA OFISI YA RUMAFRICA
Kikundi cha kusaidiana cha ambacho kimewakusanya waimbaji wa nyimbo za Injili, wajasiriamali, wafanyakazi, na watu mbalimbali kiliweza kukutana katika ofisi za Rumafrica na kuweza kujadili maswala mbalimbali ikiwa pamoja na kutafuta jina la kikundi hicho na jinsi gani kikundi hicho kitaongozwa.

Kutoka kulia, Mwenyekiti Rulea Sanga,Uhamasishaji Enoce, Katibu Leah Mwankundile, Maombi Emmanuel Dobogo

Kikao kilifunguliwa kwa maombi yakiongozwa na mtumishi wa Mungu, Egid Chang'a na baadae kikao kiliendelea kama kilivyopangwa. Walioweza kufika siku hiyo ya tarehe 09/03/2015 ni Rulea Sanga, Egid Chang'a, Emmanuel Dobogo, Tumaini Njole, Enoce na Leah Mwankundile.

Kikao hicho kiliweza kupata jina la kikundi na kuitwa USHINDI na kabla ya jina hilo kilikuwa kinaitwa Rumafrica. Baada ya kupata jina hilo la kikundi, uchanguzi wa viongozi wa muda ulifanyika na ikaonekana Rulea Sanga kuwa Mwenyekiti, Tumaini Njole kuwa Mhasibu, Leah Mwankundile kuwa Katibu, Egid Chang'a kuwa kiongozi wa nidhamu na Enoce kuwa kiongozi wa kuhamasisha maswala yanayotakiwa kufanyika katika kikundi hiki.

Kikundi kimetokana na mtandao wa Watsap ambapo watu waliweza kufamiana kwa njia ya kutumiana ujumbe na baadae wakaona kuna umuhimu wa kufamiana zaidi na kuweza kusaidiana kwa mambo mbalimbali badala ya kuwa watu wa kuchart tu.

Kwa sasa kikundi hiki kimefikia hatua kubwa sana na kiko katika harakati za kwenda hatu nyingine kubwa kwaajili ya kusaidiana na hapo baadae kinategemea kuifikia jamii yenye uhitaji na kusaidiana. Kama ungependa kujiunga unaweza kuwasaliana na Katibu wa Chama hiki Leah Mwankundile  kwa simu +255 656 219 865.
 Kutoka kulia ni Katibu Leah Mwankundile, Kiongozi wa Nidhamu Egid Chang'a, Kiongozi wa Uhamasishaji Enoce, Kiongozi wa Maombi Emmanuel Dobogo
 Tumaini Njole (kushoto)

  Kutoka kulia ni Katibu Leah Mwankundile, Kiongozi wa Nidhamu Egid Chang'a, Kiongozi wa Uhamasishaji Enoce, Kiongozi wa Maombi Emmanuel Dobogo na Muhasibu Tumaini Njole

MUNGU ANAZIDI KUONEKANA KATIKA HUDUMA INAYOTOLEWA NA RUMAFRICA

Mungu amekuwa mwema katika ofisi hii ya Rumafrica. Tumemuona Mungu akibadilisha maisha ya wafanyakazi wa Rumafrica na akibariki kazi zake. Mungu ni mwema na atazidi kuhimidiwa milele. Rumafrica imekuwa ikijihusisha sana na kutangaza jina la Yesu Kristo kwa njia ya mitandao na kuhakikisha kumtangaza yule anayefanya kazi ya Mungu dunia nzima. Mungu amekuwa mwema kwani kwa kupitia huduma hii Rumafrica imeona mkono wa Bwana.

Kuna mengi tunafaidika kufanya kazi ya Mungu, kwani tumetambulika na Yesu Kristo, watu wengi duniani wameijua huduma hii. Tumekuwa tukipokea simu mbalimbali kuhusiana na huduma yetu hii wakitupongeza na wengine kukosoa pale tunapokosea. Tunawashukuru sana kwa maoni yenu.

Rumafrivca imekuwa ikijhusisha na kutengeneza matangazo kwa njia ya Posters, Bronchure, Business cards, Billboards, Banner, Branding, CD Covers, ID, Magazine, Letterhead, kupiga picha za mnato na video, keyholders n.k

Rumafrica inapenda kuwashukuru bloggers wote Tanzania na nje ya Tanzania ambao wamekuwa bega kwa bega kutafuta habari za Mungu. Rumafrica imekuwa ikipata taarifa zingine kwa kupitia blogs za watu wengine kama blogu ya
1. Samsasali 2. Uncle Jimmy 3. John Shabani 4. K Junior 5. Joyce 6. Gospel Vision 7. Strictly Gospel 8. Vituko vya mitaa 10. Mc Chavala na wengi.

Pia ninamshukuru sana Nabii Flora amekuwa msaada wangu mkubwa katika huduma hii. hata tulisemwa maneno magumu ya kukatisha tamaa ya KIIMANI alionekana akitutea kimaombi. Mungu alinde maisha yake yawe marefu
 Rumafrica inatoa shukrani kwa familia ya marehemu Amir Sanga ambaye ni kaka yake na mmbeba maono ya Rumafrica kwa support yake kubwa kimaombi.

Imeandikwa na Uongozi wa Rumafrica