SAFARI ILIKUWAJE?
Tunamshukuru Mungu kwa kutulinda na kutufikisha salama jiji Lagos Nigeria kwa Nabii TB Joshua.
Safari yetu ilianzia jijini Dar es Salaam mida ya saa 2 usiku kuelekea Ethiopia Addis Ababa, tulifika Ethiopia mnamo saa 7:00 mchana na baada ya hapo tukakaa airport kwa muda wa masaa matatu tukisubiria ndege ya kwenda Nigeria-Lagos. Muda ulipofika tuliingia katika ndege kuelekea Nigeria. Tulipofika katikati ya Nigeria na Ethiopia (Cameroon) , rubani wa ndege akatangaza kuwa katika ndege kunatatizo la oil inavuja (oil reckage). Wahudumu wa ndege wakatuambie tufunge mikanda vizuri maana muda wowote ule ndege inaweza kudondoka. Na hii ni kutoka na ndege kuyumba sana ikiwa inalalia upande mmoja tena niliokuwepo mimi (upande wa kulia). wahudumu wakarudi kwenye vyumba vyao vya nyuma ya ndege, screen zote zikazimwa.
Baada ya kupewa hizo habari watu walianza kuwa na wasiwasi sana na wengine wakaanza maombi. Ndege ikaanza kuyumba huku inashuka taratibu. Tunamshukuru Mungu Rubani alifanikiwa kuigeuza ile ndege na kuelekea tulikotoka Ethiopia kwababu Cameroon na Ethiopia ni jirani ukifananisha Cameroon na Nigeria. Hali ilikuwa ngumu sana, watu wakanza kulia na wengine kukazana kuomba. Mungu akatusaidia na kufanikiwa kufika Ethiopia Airport ambapo watu walilazimika kushuka na kuunganishiwa ndege nyingine.
Mungu alionekana "live" akiwatetea watumishi wake ambao walikuwa wakielekea kwa Nabii TB Joshua wakitokea Tanzania. Kwa akili ya kawaida ni ngumu sana kuamini kilichotokea katika safari hiyo. Mungu aliokoa roho za watu takribani 400 ambao wangepoteza uhai wao au kuumia kama ajali ingetokea.
Muda mchache tuliunganishiwa ndege nyingine kuelekea Nigeria ambayo ilitufikisha salama na baada ya kufika airport tulipokelewa na wenyeji na kuelekea katika mabasi yaliyokuwa yanatusubiri. Mabasi hayo yalitupeleka mpaka kanisani kwa TB Joshua (SCOAN of Synagogue) ambalo lipo mjini Lagos.
Tulipokelewa na wainjilisti na watumishi mbalimbali, tukakarishwa eneo la Playerline na mabegi yetu. Walituombea tukiwa pale na kumshukuru Mungu kwa kutufikisha SCOAN salama. Baada ya kumaliza zoezi hilo tulipelekwa sehemu ya kulala ili kuhifadhi mizigo na baadaye tukapelekwa dinning Hall kwaajili ya chakula cha usiku.
Haya ndiyo mambo yaliyotokea kwetu toka tulikotoka Tanzania, Dar es Salaam kuelekea Nigeria-Lagos.
Siku ya pili tulishinda hostel na kutembezwa sehemu chache. Na baada ya kutembezwa tuliendelea na ibada za kila siku, na sisi tuliokuwa tumealikwa tulipata muda wa kuongea naye na kutuambia mambo fulani kwaajili ya maisha yetu (ni iri yangu mdau). Tulikaa SCOAN kwa muda kama wa wiki nzima tukila na kulala kwa gharama zake.
Siku ya pili tulishinda hostel na kutembezwa sehemu chache. Na baada ya kutembezwa tuliendelea na ibada za kila siku, na sisi tuliokuwa tumealikwa tulipata muda wa kuongea naye na kutuambia mambo fulani kwaajili ya maisha yetu (ni iri yangu mdau). Tulikaa SCOAN kwa muda kama wa wiki nzima tukila na kulala kwa gharama zake.
UNASEMAJE KUHUSIANA NA TB JOSHUA?
Muache Mungu aitwe Mungu. Tunamshukuru TB Joshua kwa kutupa upendeleo wa kuonana naye uso kwa uso na kwa jinsi alivyojitolea kutulipia gharama zote za kutusafirisha kutoka Tanzania mpaka Nigeria SCOAN Synagogue na kutugharamia chakula na malazi kwa kipindi chote tulichokuwa Nigeria.
Mtumishi wa Mungu anafanya kazi ya Mungu kwa Moyo wake wote na akili zake zote. Ni mtumishi anayependa sana kusaidia watu wasiojiweza na wenye matattizo mbalimbali. Hapendik kuona mtu unalegea katika kazi ya Bwana.
Nitazidi kukuletea mafundisho tuliyoyapata kutoka kwa Nabii TB Joshua, ila kwa sasa ningependa kuwaonyesha tu yale aliyotufanyia Watanzania.
Ewe mdau wa blogu yangu naomba uangalia jinsi alivyotuhudumia. Ila kuhusu tuliyoambiwa na Nabii TB Joshua ni siri yetu. Mungu akubariki sana.
Safari mpya kulekea Nigera baada ya kurudishwa Ethiopia Adis Ababa kutokana na tatizo la ndege
Rulea-ndani ya ndege baada ya kurudishwa Adis Ababa
Ndege iliyokuwa na matatizo ya kuvujika kwa oil ikiwa Ethiopia Adis Ababa
Rulea-nikishuka baada ya kurudishwa Ethiopia kutoka na tatizo la ndege kuvuja oil angani
Emmanuel Mabisa akielekea katika basi la abiria katika aiport ya Adis Ababa- Ethiopia
Rulea-Katikati nikiwa ndani ya basi la abiria-Ethiopia
Emmanuel Mabisa akielekea lkatika basi la abiria Ethiopia Airport
Nikiwa katika Aiport ya Adis Ababa nikisubiroia ndege nyingine ya kunisafirisha kuelekea Nigeria-Lagos
Nikiwa Airpot, choka mbaya
Nikiwa katika korido la ndege ya Ethiopia, tayari kwa safari ya Nigeria
SAFARI YA NDEGE
KUTOKA DAR - ETHIOPIA ADISS ABABA
Chakula katika ndege ya ETHIOPIA
TUKIWA NIGERA SCOAN
SCOAN Synagogue-Nigeria Lagos upande wa mbele
Watanzania wakiwa sehemu ya mapokezi inayoitwa "Prayer Line" mara baada ya kufika Nigeria, siku ya kwanza
TUKIELEKEA KANISANI KATIKATI YA WIKI
Hii ndio Synagogue
Emmanuel Mabisa wa pili kutoka kulia akionyesjha SCOAN Synagogue
Mabisa akiwa katika Prayer Line
Eneo la maombezi linaitwa Prayer Line. Pia ni sehemu kwa wageni wanaotembelea SCOAN
Mabisa akiingia ndani ya SCOAN Synagogue kwa mara ya kwanza
Rulea nikiingia ndani ya Synagogue kwa mara ya kwanza
Ndani ya Synamgogue karibu na madhabau
Hii ninayoonyesha ni A/C ya kanisa ambayo iko karibu sana na madhabau
Nikiwa jukabisa ambakp watu wengine hukaa katika ibada
Hawa waliokaa ni wengine kutoka nchi mbalimbali, Rulea Sanga nikiwa nipiga koti jeusi upande wa kushoto kati ya hawa waliosimama
SIKU YA IBADA-JUMATATU
Nikiwa na Mtanzania mwenzangu kutoka Moshi-Tanzania
Hii ilikuwa ni siku ya Ijumaa wakati wa mkesha
Tukimsifu Mungu
PICHA ZA KUOMBEWA KUTOKA KWA WATANZANIA
Picha za watu wenye uhitaji kutoka kwa Grac Wangwe na Neema
TUKIWA IBADANI
SIKU YA MATEMBEZI
Sehemu ambayo wanatengeneza mikate kwaajili ya wafanyakazi na wageni na wenyeji pia
Sehemu ya fundi seremala
Tukielekea sehemu ya wanyama anaowafuga TB Joshua
Dada kutoka South Africa (kushoto) akiwa na dada kutoka Ethiopia
Sehemu ya mifugo
Rulea Sanga akipata maji yenye upako ambayo hugawia getini bure
Emmanuel Mabisa (kushoto) akiwa na Frank kutoka Dar es Salaam pamoja na mtoto wa cordinator wetu Martha wa Masaki Dar
Ujumbe wenye kukutia moyo na kukuweka karibu na Mungu
Rulea Sanga akiwa ndani ya Synagogue floor ya juu
Wageni wakiwasikiliza watengenezaji wa mikate, jinsi gani wanatengeneza
Baadhi ya mashine
Sehemu ya kuhifandhia mikate
Timu ya mpira wa miguu ya TB Joshua, inasemekana baadhi ya yao ni watu wanaotoka katika familia duni na wageni ni yatima, na wanalelewa na TB Joshua
Walinzi wa SCOAN Synagogue
Ngamia zinazofugwa na TB Joshua
Gari za kubeba wageni za kanisani zikiwa zimepigwa stickers zenye upako
Plate Number yenye jina la SCOAN
Frank (kulia) Mtanzania aliyefika SCOAN
Tukielekea Kanisani
SEHEMU YA KULALA
Blogger Rulea Sanga akitafakari baada ya kukosa net ili imsaidie kurushe matukio ya Nigeria
Mabisa akiwa amejipumzisha
Mabisa akijiandaa kwenda ibadani siku ya jumapili
Rulea Sanga wa pili kutoka kushoto, nikiwa tayari kwenda Ibadani siku ya Jumapili
Makaranga akivishwa tai siku ya jumapili
SEHEMU YA NJE YA DINNING
Mabisa akiwa katika pozi baada ya kupata chakula cha mchana
Rulea Sanga nikiwa nje kidogo ya bweni, na haya ni magari ya Nabii TB Joshua
SEHEMU YA KULIA CHAKULA "DINNING"
Tukiwa Dinning Hall
SAFARI KUELEKEA TANZANIA ILIANZIA HAPA
Rulea Sanga (kulia) na Omega Assey
Tukipelekwa Airport ya Nigeria
Mbele ni Airport ya Nigeria
Kanisa la Kilutheri
TUKIWA NIGERIA LAGOS KUELEKEA ETHIOPIA
Jane P Mkony akiwa katika korido la kuingia katika ndege
akiwa bado koridoni
Jane P Mkony
Frida Gugu
Rulea Sanga
Emmanuel Mabisa
Rulea Sanga
Lisabela Ifiga
Isabela Lifiga
Naburudika
Tukimtafakari Mung
Emmanuel Mabisa akiwa ndani ya ndege ya Ethiopia akipiga msosi
TUKIWA ETHIOPIA KUELEKEA TANZANIA