RUMAFRICA Magazine

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NDOTO

NDOTO: NIMEOTA NIMEKUTANA NA RAIS DKT.  POMBE MAGUFULI NA MSAANI  WA BONGO FLEVA NA MWANAMITINDO MAARUFU TANZANIA JOKATE
Usiku wa kuamkia Alhamisi ya tarehe 02.01.2018, Rulea Sanga  nimeota ndoto niko chumbani kwangu nimelala, mara Emmanuel Mabisa akaingia chumbani kwangu akiwa na IPAD. Emamanuel Mabisa akanionyesha video ya Wema Sepetu (mhhhh!!) baada ya kuona ile video aka.....(mmmhhh). Baada ya kumaliza kunionyesha ile video, akaingia Jokate chumbani. Nilishangaa kumuona Jokate kwasababu ni mtu maarufu sana, basi tukamuonyesha ile video ya Wema Sepetu, Jokate akawa "interested". Baada ya kukaa naye kwa muda mrefu, Emmanuel mabisa akaniaga kuwa anaondoka. Nilibaki na Jokate chumbani tukiangali video ya Wema Sepetu.


Baada ya muda tulitoka nje, na Jokate akaniaga kuondoka. Nikiwa nje peke yangu akaja kaka yangu Mch. Burton Sangana tukawa tunajadili jinsi ya kwenda kanisani. Nikiwa nje ikaja mvua kali sana na baadae kukatika, ila kuliwa na maji yakitiririka sana karibu na nyumba tunayoishi. Nikiwa bado nipo nje na kaka yangu akatokea Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mzee mmoja. Nilishangaa kumuona Rais nyumbani kwangu, nilitamani kuongea naye, nilijitahidi kumuongelesha mara akanijibu na tukaanza kupiga story. Tukasogea kwenye eneo la mavuriko wa maji, nikachukua kamera na kumpiga picha. rais alipomaliza kuangalia mafuriko alitamani kuondoka na mimi pamoja na yule mzee kwenda kununua pombe ya kienyeji ili anywe, nami nikamwambia mimi nimeokoka sinywi pomba, akanijibu, "Basi sawa". Akaniomba tuondoke eneo la nyumbani na kwenda eneo jingine tuka "relax". Tuliondoka eneo hilo..baada ya hapo nikaamuka usingizini

NDOTO: NABII  TB JSOHUA WAKATI AKIHUBIRI NA KUTABIRI TANZANIA GHOROFA MBILI ZADONDOKA
Usiku wa kuamkia Jumanne 24.10.2017 Rulea Sanga nimeota ndoto Nabii TB Joshua yupo Tanzania akihubiri katika kanisa lake analolijenga hapa Tanzania. Nabii TB Joshua alionekana akiwa na vumbi kisogoni huku akiwatabiria watu. Lengo la Nabii TB Joshua kuja Tanzania ilikuwa ni kusimamia ujenzi wa kanisa lake. Wakati akihubiri nikaona jingo ghorofa karibu na ghorofa na TANESCO Ubungo Tanzania likidondoka. Kipindi ghorofa likidondoka Nabii TB Joshua alikuwa bado akiendelea na kuhubiri huku akitabiri.
 Nabii TB Joshua


Baada ya muda mfupi ghorofa karibu na kanisa lake likadondoka, Nabii TB Joshua akasimama kuhubiri na kutabiri, akajawa na hofu na akanituma niende karibu na lile ghorofa lililodondoka. Nikiwa naelekea kwenye lile jingo, njiani nikakutana na watu wakiwa wamewabeba watu walioumia katika lile jingo wakiwapeleka kwenye magari ya wagonjwa, lakini nilishangaa kumuona mama mmoja akiwa amekatwa mkono wa kulia akiwa hana msaada akigalagala chini huku akijiviringisha akilalamika na maumivu; nilimpita Yule mama na kufika eneo la tukio.

Nilipofika mahali pale nikakuta watu watengeneza duara na katikati ya duara kwenye nyasi chini kuna kitu mama mafuta yamemwagwa, miguu ya kuku waliopikwa, na lishangazwa kuona eneo hilo hakuna hata damu ya watu walioumia katika ajali.  Baada ya hapo niliondoka katika eneo nikielekea kanisani kwa Nabii TB Joshua. Wakati nipo njiani nikawa najaribu kupiga picha ya ghorofa lililobomoka kwa njia ya “selfie” lakini nikawa sipati picha ya jingo bali najiona mwenyewe. Baada ya hapo nikaamuka ndotoni.

..............................................................................................................................


NIMEOTA NDOTO NIMEKUTANA NA NABII TB JOSHUA NIGERIA KANISANI KWAKE SCOAN

Usiku wa kuamkia Jumatatu 26.06.2017 nimeota ndoto nikao kanisani kwa Nabii TB Joshua SCOAN Nigeria na baadhi ya watanzania na mmojawapo ni mwinjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Nikiwa pale nilimuona Nabii TB Joshua akihubiri na baada ya kumaliza kuhubiri kipindi cha kwanza cha ibada alitoka nje, na nikabahatika kuonana nae na kujisalimiana.
Nabii TB Joshua

Nilijitambulisha kuwa mimi ni Yule kijana kutoka Tanzania ambaye mwaka 2012 alinaialika kanisani kwake. Nabii TB Joshua baada ya kunikumbuka alitamani kuwa rafiki yake. Niliondoka naye mpaka nje ya kanisa, tukazunguka hadi nyuma ya kanisa ambako huko niliona shimo kubwa sana, nikaanza kumuuliza swali na kumshauri.

Ushauri wangu, nilimuambia, anaonaje akapanua kanisa lake liwe kubwa zaidi, akanijibu; inawezekana na yuko katika mpango wa kuliongeza kanisa; nikamuuliza kama ataongeza kanisa hili shimo itakuwaje? Hakunijibu kabisa. Tukaondoka tukaelekea eneo jingine la kanisa, tulipofika pale nikamuomba Nabii TB Joshua anisaidie na mimi nianze kufanya huduma katika kanisa lake kama mtu wa IT; hakujibu lakini alichokifanya akanishika mkono na kuingia katika chumba kilichojaa vitabu, akachukua Kamusi (Dictionary) ya Kiswahili, gamba lake (cover) lilikuwa na rangi ya Blue na nyeupe ambalo limeandikwa KISWAHILI – ENGLISHI. Nilichukua ile kamusi na kuanza kutafakari kwanini ameamua kunipa Kamusi?

Na kwanini hajanijibu kuhusu swali langu la kufanya huduma katika kanisa lake? Nilibaki nikisikitika moyoni. Nikiwa natafakari, wazo likanjiia na kugundua kuwa Nabii TB Joshua alikuwa na lengo la mimi kunjifunza Kiingereza ili nifanye kazi kwa viwango vya kimataifa. Baada ya hapo niliamuka usingizini 3 asubuhi.

..............................................................................................................................

NIMECHELEWA KUFANYA MTIHANI
Usiku wa kuamkia tarehe 12.02.1014 siku ya Jumatano nimeota ndoto niko Mafinga Iringa. Nimeota ndoto nimetoka nyumbani kwa kaka yangu  marehemu Amir Sanga nikielekea sokoni kuwa naelekea kufanya mtihani wangu wa kumaliza chuo. Nilipofika sokoni  nilimuona mke wa mjomba wangu (Jomba) akiwa amegeukia dukani kwake. Nilijitahidi kumpita bila ya kumsalimia kwani nilikuwa na haraka ya kuwahi kufanya mtihani. Mke wa mjomba wangu aligeuka na kutaka nimsalimie, nilimsalimia na baada ya kumsalimia nilielekea dukani kwa kaka yangu nikiwa na hofu kubwa kwani muda wa kufanya mtihani ulikiwa umepita. Nilipofika dukani kwa kaka yangu nilimsalimia naye aliniitikia kwa upendo huku akitabasamu, nilijisikia aibu sana na nilisita kumwambia kuwa nimechelewa kwenda kufanya mtihani. Nilmuaga kaka yangu na yeye alinitakia mafanikio mema.

Niliondoka mbio kuelekea katika chumba cha mtihani. Nikiwa njiani nilikutana na watu nikawauliza, ni wapi wanafunzi wenzangu wanafanyia mitihani? Watu wale hawakunijibu, nikaanza kuhangaika kutafuta mahali walipo ili niungane nao kufanya mtihani. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu,nilionana nao wakiwa wameshatoka katika chumba cha mtihani. Niliumia sana kuona nimechelewa kufanya mtihani. Wezangu walionekana wakiwa na furaha huku wakijadiliana yale waliyoyakutaka katika mtihani wao.

Niliingia katika chumba cha mapokezi na kumuona mzee mmoja ambaye anahusika na kuwaruhusu watu kuingia kufanya mtihani. Nilimueleza kuwa mimi nimechelewa kufanya mtihani na ninatamani kufanya mtihani. Yule mzee aliniambia subiri kidogo nione ili ni jinsi gani ya kukusaidia. Nikiwa namsubiria, nilimuangalia sana Yule mzee, naye alionyesha sura ya kutaka kuhongwa fedha ili anisaidie. Nilijiuliza, inawezekanaje kuingia kufanya mtihani wakati muda wa kufanya mtihani umeshapita na wasimamizi wa mtihani wameshachukua karatasi za mitihani? Nilibaki na kiulizo kichwani lakini nikawa na tumani kutoka kwa Yule mzee kwani alinambia nisiwe na wasiwasi atanisaidia.

Moyo wangu uliumia sana tena sana kukosa kufanya mtihani wa mwisho. Nilkuwa na masawali mengi sana kwani huo mtihani ulikuwa ni mtihani wa mwisho wa kuhitimu chuo, na kama mtu atakosa kufanya anarudia mwaka. Pia nilijiuliza hivi kaka yangu akisikia sijafanya mtihani kwa kosa  la kuchelewa atanichuliaje? Niliumia sana moyoni huku nikiona aibu kwa marafiki zangu walioonekana kuwa na furaha kutokana na ule mtihani kuwa mrahisi.

Pia nilikuwa binafsi sijajiandaa nikimaanisha sikusoma kwa muda mrefu mpaka siku ya mtihani, kwahiyo hata ningewahi bado ningeshindwa ule mtihani kwani sikujiaandaa kabisa kutokana na mishemishe zangu za utafutaji wa fedha mitaani. Ulikuwa wakati mgumu sana. Baada ya hapo niliweza kuamka usingizini huku moyo wangu ukiwa unaumia sana na kutotamani ile ndoto kwani iliniumiza sana.

----------------------------------------------------------------

NIMEOTA NDOTO NDEGE IMEDONDOKA

Usiku wa kuamkia Jumatatu ya tarehe 19.01.2014 Jumapili Rulea Sanga, nimeota ndoto watu wako baharini wanaogelea, nilipoaangalia juu niliona ndege ya abiria ikishuka chini kwa kukosa nguvu. Mara baada ya muda ile ndege ilidondoka chini. Nikiwa na rafiki zangu na rubani wa ile ndege pembeni mwa bahari alianza kuelezea huku akitabasamu na bila ya hofu yoyote juu ya ile ajali ya ndege. Baadhi ya watu walipoteza maisha na wengi walikuwa wakitapatapa majini wakitaka kuokolewa.
-------------------------------------------------

NIMEOTA NIKO KARIBU NA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Usiku wa kuamkia tarehe 28.12.2013, nimeota ndoto niko Mafinga na nikiwa Mafinga, nimeota niko sokoni na wenzangu katika lori lililopaki sokoni karibu na duka la marehemu kaka yangu Amir Sanga. Katika hilo lori kulikuwa na watu ambao walionekana ni marafiki zangu kutokea huku Dar ninakoishi kwa sasa. Niliwaonyesha rafiki zangu store ya duka la kaka yangu ambayo ilikuwa ni duka la zamani la mjomba wangu ambaye kwa sasa ni marehemu anayeitwa Lusani Sanga ( alimuuziaaga kaka yangu kipindi ni mzima), niliwaambia hao rafiki zangu, “Hii ni store ya kaka yangu, mmeiona sasa?” hawakunijibu walizidi kuangalia tu hiyo store

Baada ya hapo nikaelekea  katika eneo la Benki ya NMB. Nikiwa pale nimeota niko na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amevalia koti la draft, shart la light blue na suruali ya blue na viatu vyeusi. Katika eneo hilo la Benki kulijengwa ofis moja nzuri sana ambayo anatakiwa Raisi Kikwete kuhamia kutokana na muda wake wa kuwa Raisi wa nchi kuisha kwahiyo anahitaji kuwa na ofisi yake binafsi.

Kushoto ni Rulea Sanga na mwigizaji wa filamu Tanzania JB
Tukiwa katika eneo hilo na watu wengi sana wakiwa wamezunguka eneo hilo na waingine wakija mahali hapo, Raisi akiwa anatabasamu alisema, “Mimi hata nikihamia hapa, siku ya kustaafu tena nikiwa katika jingo hili au ofisi hii mpya basi mtatoboa mlango mwingine katika jingo hili hili wakutokea na huko mtajenga jengo lingine la kuhamia, na huo ndio utaratibu wa mtu anayestaafu” Raisi baada ya kusema hayo niliamka kutoka usingizini.

-------------------------------------------------------------

NDOTO NIKIWA NATEGENENEZA BENDERA YA ISRAEL NA TANZANIA YA MTUMISHI WA MUNGU TANZANIA 25.12.2013

Usiku wa kuamkia  26.12.2013 nimeota ndoto niko katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni na nikiwa pale nilikuwa nimesimama katika nguzo moja nikimuangali Mchungaji Getrude Rwakatare. Baada ya yeye kuniona aliniita na kutaka nimtengenezee bendera ambayo itaunganisha bendera ya Taifa Israel na Tanzania. Katika maongezi kuhusiana na bendera kuwakawa na ubishani kidogo wa kutaka bendera kuwa bora zaidi. Nilimshauri Mchungaji Rwakatare kuwa angejaribu kuweka anuani itakayokuwa  inaonyesha kanisani lake lilipo katika hiyo bendera na maandishi yawe ya rangi nyekundu http://4.bp.blogspot.com/-MPZxNPlMieU/Uh0mHEx5y4I/AAAAAAAASBY/pPMJxU9f648/s640/DSCN6289.JPG
Nikiwa nikiongea naye nilikuwa nikionekana kama nina hasira sana wakati Mchungaji Rwakatare akiwa na muonekano wa furaha na kuniheshimu sana. Kichwani kwangu nikawa nawaza juu ya yale yaliyotokea katika nyumba yake mpya ambayo anaishi sasa ambayo ilinisababishia matatizo na  maelewano kati yangiu na yeye kutokuwa mazuri.

Baada ya muda tukakubaliana na mimi nilikubali kumtengenezea na bendera ilikuwa kama hii. Dhumuni la Mchungaji Rwakatare alitaka bendera hii itumike kanisani kwake ambapo waumini watakuwa nazo wakati wa ibada.
Hii ndio bendera…


----------------------------------------------------------------

NDOTO YA KUPAMBANA NA MAPAKA, PANYA NA MISKULE YANITISHIA AMANI..ILA YESU ALINITETEA
Usiku wa leo kuamkia Jumanne 24.12.2013, nimeota ndoto mbaya sana ambayo nashindwa kujua ni kwanini…Nimeota niko chumbani kwangu nimelala katika kijiji cha Mtili “A” kilichoko mkoa wa Iringa.  Nikaona maji yanachuruzika kuelekea kwenye godoro nililotandika chini ya sakafu.

Hapa ni sebuleni nilipolala baada ya kujisikia uvivu kulala chumbani...Ndoto zote za ajabu zilinikumba hapa sebuleni...

Muda kidogo nikamuona paka mwenye madoa meupe na meusi ameingia kupitia dirisha lililokuwa wazi. Nikachukua fimbo na kuanza kupiga, paka Yule akakimbia kwa kupitia tundu dogo la mlango wa sebuleni na kwenda nje. Nikiwa bado nashangaa mara paka wa pili akaingiawa rangi nyeusi, nikaanza kupambana naye kwa kumpiga na fimbo lakini sikufanikiwa kumua akakimbia nje kwa kupitia tundu hilo hilo alilopitia paka wa kwanza. Sijakaa sawa mara  paka wa tatu akaingia nikapambana naye akakimbilia kwenye chumba cha mama (ambaye kwa sasa ni marehemu); nikamuasha mama yangu, mama yangu alipoamka tu paka akakimbia na kutokea tundu lile lile la subuleni.

Mama akiwa hospitalini Mbeya na siku ya pili akawa ananiacha duniani na mpaka sasa sijamuona tena...

Nikamuomba mama na kaka yangu Burton (ambaye alikuwa akimlea mama yangu uzee wake mpaka anatuaga dunia)  kuanza maombi tukawa tunasali huku tumeshikana mikono. Wakati tupo katika maombi kikatokea kitu kidogo kama panya, nikachukua fimbo ambayo ilikuwa ikionekana kama mwiko mrefu wa kusongea ugali nikaanza kukipiga kikageuka na kuwa kopo la soda kama ya Sprite.


Kopo la sprite


 Baada ya kumaliza na huyo panya mara  paka wawili wakatokea tukiwa sebuleni mimi, mama na kaka yangu wakati tukiomba na kukemea haya matukio yaliyokuwa yakitutokea. Mimi nikaanza kumpiga Yule paka mmoja aliyekuwa na madoa meupe na meusi kama madoa ya chui, naye akakimbilia katika chungu kilichowekwa na mama yangu kwenye kona ya nyumba. Nikapambana Yule paka kwa kwa kumkandamiza na mwiko akiwa kwenye kona naye akapata upenyo akakimbia, wakati huo  mama na kaka wanapambana na paka mwingine lakini hatukufanikiwa kuwaua au kuwaangamiza, nao wakakimbia tukabaki tunashangaa ni kwanini haya yanatokea. Nikaanza kusali na ninakumbuka maneno niliyokuwa nikitamka wakati ninasali, nayo ni kama haya. Ninakushukuru Mungu kwa yte unayofanya katika maisha angu, umenipa uzima na furaha, Mungu wewe ni mwema kwangu. Angalia haya yanayotutokea kwa sasa, ninaomba unisadie…Mfano wa paka...

Nilipomaliza kuomba, mara  nikaona mlango ambao hao paka walikuwa wakitokea umefunguka, nilipoangalia nje niliona gari aina ya ESCUDO nyekundu limegonga ukuta wa nyumba upande chumba changu, nikamuona dereva aliyegonga ule ukuta akiwa anahangaika kugeuza gari ili akimbie huku akitabasamu na mara akafanikiwa na kukimbia kuelekea kijiji cha jirani cha  Ifwagi upande wa mashariki.

Gari yangu kipindi nimepata ajali ya tairi kuchomoka maeneo ya mwembechai Dar nikielekea kazini
Posta


Ukuta ulionekana kubonyea kwa ndani  na wala haukudondoka na nikaenda ndani kuangalia kama kuna uharibifu wowote zaidi ya kubonyea, nikaona ule ukuta  kwa ndani uko salama na ukuta haujabonyea kwa ndani. Nilivyoona hivyo niliumia sana na nikaanza kupiga kelele ili watu wanisaidie kumkamata huyo dereva huku nisema,  kamateni huyo….kamateni huoyo…. lakini hakuna alionyesha kunisaidia. Nikaingia ndani na kumueleza mama na kaka yangu Burtoni ya kwamba nyumba imegongwa, hawakunijibu walionekana kusikitika sana.

Nikaingia chumbani kwa mama na kuona vitanda viwili kimoja kikiwa na mama mmoja amelala na huyo mama wa kanisani kwa Nabii Flora na kitandani kwa mama yangu kuna vitu viwili vya rangi ya blue na nyeusi na chumba kikiwa na mwanga wa kutosha huku kikitoa harufu ya mikojo. Tukaanza maombi , wakati tunaomba mara vile vitu viwili vikageuka kuwa miguu yaani nyayo za watu. Nikamshukuru  Mungu kwa kuwa niliona amejibu maombi yetu na kumkamata adui yetu kwa kile kitendo cha vitu kugeuka na kuwa nyayo za watu.
Baada ya muda mfupi,  wakati tunaendelea na maombi mara nikaona misukule ya watu miwili wa jinsia kiume wamelala kitandani kwa mama yangu wakiwa wamepakwa rangi nyeupe na hawajavaa nguo zaidi ya vichupi vilivyochakaa sana, midono yao imekunjamana na wanaonekana kama tahira. Nikaichukua ile misukule miwili kwa mono wangu mmoja wa kuume nikiining’iniza juu huku nikikimbia kuelekea nyumbani kwa kaka yangu mkubwa Yohana kwaajili ya msaada, wakati huo huo nikipiga kelele nikisema, nisaidie…nisaidieni… lakini hakuna mtu aliyeonekana wa kunisaidia.

Nilipofika kwa kaka yangu nikagonga mlango wa chumba cha kulala watoto wa kaka yangu (Yohana)  na wakati nagonga nikasikia sauti za watu ndani ya hicho chumba wakiongea lakini hawafungua mlango kunisaidia. Nikaenda jikoni huku nimeshika misukule nikamkuta shemeji yangu (mke wa kaka yangu Yohana) anasonga ugali, nikawa naomba msaada wa kunisaidia huku nimeshika misukule lakini hakuonyesha kunijali. Nikaamua kurudi nyumbani huku nikisikitika sana. Nilipofika tu, nikamuona mama yangu na kaka yangu wakisali huku wakilia sana, na mimi nilishikwa na uchungu na hasira sana dhidi ya haya yaliyokuwa yakitutokea. Nikiwa na mama yangu na kaka yangu mara ile misukule ikageuka na kuwa viatu vya blue na vyeusi, nilisikitika sana na kuona juhudi za kuomba hazija zaa matunda. Nikaungana  na mama yangu na kaka yangu kuomba. Tukiwa katika maombi watu wakaanza  kusanyika wengi wakituzunguka.

 Wakati watu wametuzunguka wakitaka kujua kitu gani kinatusubu kwa wakati huo, Mama akaanza kuimba wimbo wa huzuni huku akicheza style ya nyimbo za Afrika magharibi au Afrika kusini ambazo mimi binafsi  huwa ninazipenda sana. Nilimuangalia mama huku nikijisikia vibaya sana na kumuonea huruma na nikiwa najiuliza kwanini hawa wachawi wanamuonea sana mama yangu  wakati mama yangu hana historia ya ubaya na mtu na ni maskini sana. Nilidondoka chini na kuanza kulia kwa uchungu huku kamasi zikinitona na machozi mengi yakinitoka, nikiwa nimeinamisha kichwa changu chini. Nilipoinuka nikamuona mdada mmoja na mkaka mmoja wamevalia nguo za Kiafrika zenye rangi nyeusi, blue, kijani na mchanganyiko wa yelo wakiniangalia kwa huruma sana, hakika nilifarijiwa nao sana, lakini sura ya dada Yule nikawa nashindwa kumuona vizuri ila mdomo wake ulikuwa umepakwa uwanja mwekundu sana na sura yake ya maji ya kunde.  Sikupenda kuinua kichwa changu kabisa kumuangalia juu ila Yule kaka nilimuona kwani yeye alipiga magoti karibu yangu akiwa akinisihi nisilie.

Baada ya hapo nikiwa nimelala shingo yangu ikawa ngumu sana kugeuka upande mwingine, ikabidi nianza maombi na mara baada ya kuomba shingo iliweza kugeuka na hatimaye mikaweza kuamka kutoka usingizini.