RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

(TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES – TCU)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

UTANGULIZI

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities’-TCU) ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council for Technical Education’ - NACTE) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board) inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:

MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”

Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinatakiwa kuwasilisha programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo wa mature entry, Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa na kuratibu utaratibu wa mitihani katika vituo maalum kikanda ili vyeti vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na hatimaye kuweza kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.

Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “Pre-entry” na “Mature Age Entry” na kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa kusudi hili utaanza mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya mitihani yao na kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.


Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-Entry” na “Mature Age Entry”.


1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo wa Pamoja (Central Admission System)


Waombaji watakaopitia mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) wamegawanyika katika makundi manne, ambapo waombaji wa kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa kama “Direct Applicants” na kundi (iv) watatambuliwa kama “Indirect Applicants”

Waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waliohitimu mafunzo ya diploma ya elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo vinavyotambulika na NACTE miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu;
Waliohitimu mafunzo ya Diploma ya Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waombaji ambao sio wa moja kwa moja (Indirect Applicants) ni wote waliohitimu kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma ya Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita (kuanzia 2009 kurudi nyuma).

1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi yao Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha maombi kupitia vyuo husika ni wenye sifa linganishi (Equivalent Qualifications) yaani wenye vyeti vya Astashahada na Diploma ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na NACTE. Ili kukamilisha udahili, wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili vyeti vyao vitambuliwe na kusajiliwa kabla udahili haujaanza.

Vyuo vinavyofundisha programu mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na Diploma ambavyo havina usajili wa NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka iwezekanavyo ili matokeo hayo yaweze kutumika katika utambuzi wa vyeti vya wanafunzi husika.

MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa kuwasilisha maombi ya udahili kwenye CAS umegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:

Kundi la Kwanza – (1 Aprili mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6), na Diploma ya Ualimu kuanzia mwaka 2011 kurudi nyuma wataanza kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30 Aprili 2012.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Comments