RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BLOGGER WA RUMAFRIKA, RULEA SANGA APATA AJALI  29 FEB 2012 MIDA YA SAA NNE ASUBUHI MAENEO YA MWEMBECHAI DAR ES SALAAM

Nikishuhudi yaliyonipata mtoto wa mkinga

Hii ni baada ya gari kuchomoka tayari ya mbele....Ilikuwa vigumu kuamini maana ndani ya gari nilikuwa peke yangu nikitokea nyumbani Sinza nikielekea ofisi za Uhamiaji Kurasini. Nilikuwa katika speed kali. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba mbele yangu kulikuwa hakuna gari lolote. Nilijitahidi kukanyaga break na haikuwezekana, gari lilikuwa likiserereka huku usukani ukiwa mgumu....Namshukuru akili yangu ilitulia na sikuweza ku-panic hata kidogo..niliamini ukiwa na Mungu kila kitu kinakuwa sawa hata ukipatwa na magumu. Gari iliendelea kwenda mbio na ikinipeleka upande wa tairi lilikochomoka....Watu walipiga kelele sana wakijua gari linaenda kuanguka au kulipuka kwa maana cheche zilitoka nyingi sana. 

Tairi lililochomoka ni la upande wa kulia

Baada ya gari kusimama wasamalia wema wakanisaidia kulivuta na kuliweka pembeni...Na mpaka sasa naongea gari liko garage...

Baada ya kutoka katika usukani, nikakumbuka kupiga picha

Kabla ya ajali, nikimaanisha usiku wa jana nimeota gari langu limelipuka moto na linawaaka moto...na kiichosababisha kuwaka ni ukosefu wa maji nyumba..Na nikiwa katika ndoto nikaoota mwenye nyumba ananiambia nizima radio inamsumbua...kutokana na nyimbo za dini zilizokuwa ziikimbwa katika kituo cha radio cha Praise Power....Na ni kweli jana usiku radio yangu usiku mzima ilikuwa iko katika station ya Praise Power radio...Haya ndiyo yaliyonisibu mwenzenu...Ahsante Mungu kwa kuniokoa..Nakupenda Mungu wangu..Mwaaaa.
 Washikaji wakiliangalia gari la mtumishi

 Angalia sehemu ya tairi


 Watu kibao wakishuhudia msala

 Balaaaaaa!!!!!!

 Hakuna wizi hapa, nisha-lock milango

 Fuluuu kuchimba

 Sehemu iliyoharibika

NASUBIRI MAUMIVU KUTOKA GARAGE

Comments