RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DINI YA RAIS WA MAREKANI OBAMA BADO HAIELEWEKI


Hivi karibuni mzozo kuhusu dini ya Rais wa Marekani Barack Obama umeibuka tena, ambapo wapinzani wake wakimhusisha na dini ya kiislamu.

Mtumishi wa Mungu Franklin Graham, mtoto wa Mwinjilisti Billy Graham alipohojiwa na kituo cha MSNBC kuhusu dini ya Obama, Alijibu ” Muulizeni yeye, siwezi kumjibia mtu swali hilo, Ninachojua mimi ni mwenye dhambi, na Mungu amesamehe dhambi zangu, Graham akasema “inabidi kumuuliza yeye, amesema yeye ni Mkristo, hivyo nami nadhani ni Mkristo” Na alipoulizwa kama Obama ni Mwislamu, akasema “hapana”

Hata hivyo Raisi Obama amekuwa akisema yeye ni Mkristo kwa msisitizo.


Comments