IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26 FEB 2012 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE LILILOKO JIJI DAR ES SALAAM
Nabii Josephat Mwingira
Na Mwandishi wetu, Rulea Sanga
Jumapili iliyopita tulijifunza Nguvu ya Mungu na kuona kazi zake. Moja ya kazi ya Nguvu ya Mungu ni Usaidizi, na leo tutajifunza kazi zingine kuhusu Nguvu ya Mungu
Kanisa la Efatha Mwnge, muonekano wa mbele geti kuu. Watu ni wengi sana katika kanisa hili..na watu wanabarikiwa sana na huduma inayotolewa mahali hapa.. Mungu akuwezeshe kufika katika kanisa hili.
B) KUMUONDOA MAHALI FULANI NA KWENDA MAHALI PA USAIDIZI.
(Ayubu 19: 25-26)
- Nguvu ya usaidizi inatusaidia kumuona Mungu wakati wa mateso ambapo Mungu hujitokeza. Hata ukiwa katika magumu utashangaa unatokea mlango wa pili.
- Nguvu ya Mungu hutokea baada ya maombi, na inakufanya wewe kuwa salama
- (Zaburi 91:1) Nguvu ya Mungu hututoa na mtego wa maadui. Hatupaswi kumwamini mtu yeyote duniani, bali mwamini Mungu
Waumini wakiwa ndani ya kanisa kabla ya Ibada ya pili kuanza.
C) NGUVU YA MUNGU NI KWAAJILI YA KUKUTOA MAHALI PA CHINI NA KWENDA MAHALI PA JUU.
- Mahali pa chini ni daraja la kuteseka kudhihakiwa na kutosaidiwa na mambo mengine kama hayo.
- (Nyakati 1:4:9-10)- Nguvu ya Mungu hutusaidia kufanikiwa na kumpa Mungu utukufu.
- Ili uwe mshindi lazima ujue siri za nguvu za Mungu, kwa mfano kama huna pesa ya posa, huna mke/mume n.k. usiombe juu ya hilo bali omba uwe na nguvu za Mungu na ukiwa nazo hizo nguvu mambo mengine yatafunguka.
- Neema ya Mungu husaidia kushinda changamoto ya maisha, kwahiyo jitahidi kuwa na nguvu za Mungu ili uyashinde hayo yanayokusumbua.
- Ukiwa na Nguvu za Mungu utaheshimika na watu wa rika zote. Utaonekana ni sukari katika midomo yao. Watatamani kila wakati kukuona na kutaka ushauri kutoka kwako.
- Maombi ya kufarijiana hayana maana sana, lakini maombi ya kukaripia adui yako yanakufanya kuwa jasiri.
Kanisa la Efatha muonekano wa nje...Kila mtu ukiomuona ana sura ya furaha na yule anayeumwa anakuwa na moyo wa matumaini.
D) NGUVU YA MUNGU NI KWAAJILI YA KUTHIBITISHA UWITO WETU, KUTUTOA KATIKA UPWEKE NA KWENDA KATIKA UTELE.
- (Nyakati 2:17:1-6) Ukimjua Mungu, amani unakuwa nayo, hofu inatoweka na unakuwa na uhakika na hicho unachokiona.
- Kumbuka Imani ni kuwa na uhakika na mambo unayoyatarajia.
Nguvu ya Mungu inakupa uhakika wa imani yako. Imani yako inafanya kazi ya kuleta kile akili inaelewa, tunatakiwa kuruhusu akili kukubali. Kazi ya akli ni kuamini kile ambacho kiko mbali na wewe na kazi ya imani ni kuleta kile ambacho kiko mbali na wewe.
- Nguvu ya Mungu inasaidia akili yako kuona ambayo akili ya kawaida haiwezi kuona na kusababisha kuweza kuona na imani kuweza kuleta.
- Mungu hawezi kukudhalilisha mpaka bali hukufanya kuwa na ulinzi.
MWISHO:
Tangazo: Kanisa la Efatha Mwenge imeanzisha huduma ya BIMA (Insurance) kwahiyo unakaribishwa katika ofisi zilizoko Nuru Center Mwenge ukakatie gari lako.
MUNGU AKUBARIKI NA KARIBU KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE UKOMBOLEWE NA YESU

Comments