RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TIMU YA GOSPEL TEAM YATAMBA KATIKA UWANJA WA SHULE YA SKONDARI KENTON SINZA MORI BAADA YA KUITWANGA TIMU YA VANKHUVA MABAO 5-0
Na mwandishi wenu, Rulea Sanga
Ni siku mbili zimepita, timu ya Gospel Team ilivyopiga bao timu ya Utumishi wa Umma kutoka ofisi ya Rais-Ikulu mabao 3-2, Jumamosi hii imegawa dozi tena kwa timu ya Vankhuva kwa kuwapiga mabao  5-0.  Wachezaji wa Gospel team walionekana kuwachanganya wapinzani wake kwa mbwembwe nyingi uwanjani  za kuwapiga chenga na washabiki kuzidi kuwazingua kwa mavuvuzela.

Baada ya mechi kuisha, makocha wa Gospel Team na Vankhuva Team  waliwasisitiza wachezaji wa pande mbili  kukaza buti kimazoezi na wasibweteke kwa haya mabao 5 na kujiona wamefika mwisho. Wachezaji waliyapokea hayo kwa mikono miwili na kuahidi kuwa watayatekeleza.

Gospel Team ni timu ambayo inajumuisha waimbaji wa nyimbo za injili, maproduza na watangazaji wa radio za Kikristo Tanzania. Lengo lao ni kumuinua Kristo kwa njia ya michezo na kuijenga na kuwaweka fit wachezaji kiafya. Mbali na hapo ni kujenga urafiki, kujuana na kuinua vipaji  kwa njia ya michezo. Mungu Ibariki Gospel Team
Wachezaji wa Gospel Team wakkimsikiliza mwalimu wao wa mazoezi.
Wachezaji wa Gospel Team wakipasha misuli kabla ya mechi

Timu ya Vankhuva wakiwa tayari kupambana na Gospel Team

 Gospel Team ikiwa na sura za mafanikio kabla ya mechi kuanza
Timu ya Vankhuva (jezi ya blue) wakisalimiana kabla ya mechi kuanza
Kazi imenza uwanjani...

 MC wa Glorious Celebration hakukosa kuliangalia pambano hili.
 Gospel Team wakiwa katika mapumziko kipindi cha kwanza
 Mzee wa Mablogu, Rulea sanga (wa pili kushoto) akiwa na goalkeeper wa Gospel Team, Silas Mbise.
Mbali na kuwa na uwezo wa kutengeneza blogu, pia ni mtalaamu wa shooting, movie editing, Graphic Design, Websites...huyu ni mzee anayejulika kwa mablogu, Rulea Sanga.
Mratibu wa Gospel Team, Erick (wa tatu kutoka kulia) akitafakari...
 Mtumishi kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Stanley (kushoto), ambaye amekuwa msaada mkubwa katika timu ya Gospel kwa kuwatibu wachezaji wanaoumia uwanjani.

 Fulu kicheko, Mtangazjai na Meneja ya Praise Power Radio ( wa tatu kutoka kushoto) akifuatilia mpambano kipindi cha kwanza. 
 Mchezaji wa Vankhuva aliyeumiza baada ya mchezaji wa Gospel team, George Mpela kuvaa kwa bahati mbaya sehemu ya ugoko.
 Hiki ni kidonda...Tunaomba maombezi yako kwa huyu mchezaji, kwani ilikuwa bahati mbaya uwanjani
 Wachezaji wa pande mbili wakipigwa picha ya pamoja baada ya mechi kuisha

MUNGU IBARIKI GOSPEL TEAM NA VANKHUVA TEAM..AMEN

Comments