RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UNAIJUA GLORIOUS CELEBRATION GOSPEL BAND????
Baadhi ya waimbaji ns wapigaji wa Glorious Celebration

Band nzuri inayovuma kwa sasa nchini Tanzania, kwa uchezaji wao wa staha na sauti zenye kusikika vyema. Kiongozi wa Glorious Celebration Band Emmanuel Mabisa, aliongea nasi machache kuhusu kazi yao na malengo waliyonayo katika kuujenga mwili wa Kristo.

Mwimbaji ,na mpigaji kinanda  wa Glorious Celebration, Danny Kibambe akimuombea dada aliyepagawa na mapepo

“Maono yetu ni kufanya huduma mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kuwahubiria Vijana Habari njema za Kristo, na pia kufanya matamasha makubwa mbali mbali”

Alkadhalika kundi hili linaundwa na waimbaji mahiri wanaosikika kwenye soko la muziki wa injili na wengine chipukizi wanasikika. Band hii inalelewa na msimamizi mkuu Bishop Mwakang’ata wa Full victory Gospel Church ya Chang’ombe Temeke, Dar es salaam.

Baadhi ya waimbaji wakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji

Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Angel Bernard ambaye ndiye mweka hazima, Chaka Mtunguja Katibu wao, Jesca Honore, Nice Marandu, Davina, Risper, Ima Malisa, Emmanuel Materu, Emmanuel Gripa, Daniel Kibambe, Arone Botto, David Silomba, Ester Peter, Paul Mwakanyamale na Mercy Denis. 

Pia kuna mtumishi wa Mungu Rulea Sanga ambaye yeye sio mwimbaji ila ni kijana anayejitahidi kuitangaza band hii kwa njia ya mtandao na amekuwa akijishughulisha na kazi ya shooting na upigaji wa picha mnato (stiil pictures).....Mungu bado hajampa karama ya uimbaji, ila anasema ana ndoto za kuwa mwimbaji wa kimataifa kwa utukufu wa Mungu.

Kwa sasa wanajiandaa kurekodi Live Dvd mapema mwezi wa sita mwaka 2012! Hapo awali wamerekodi video ya album yao ya kwanza NIGUSE, unaweza kufarijika kwa kusikia wimbo huu wa NIGUSE.

Mpaka sasa wametimiza mwaka mmoja tangu wameanzisha bendi yao na wametoka na album ya NIGUSE….hata hivyo kama watu walivyozoea kila Ijumaa kuwaona THE ATRIUMS HOTEL, kwa sasa itakuwa wanamtukuza Mungu kila ijumaa ya mwisho wa mwezi, viwanja vile vile.
Tanzania tunajivunia kuwa na waimbaji kama hawa!

Comments