RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RATIBA YA GOSPEL STAR SEARCH (GSS) SEASON 2

Ule Mchakato wa Kumsaka Waimbaji wa Muziki wa Injili wenye Kipaji, umeingia katika hatua yake ya Pili, baada ya siku ya leo, Mwenyekiti na Mratibu wa Gospel Star Search 2012, Pastor Harris Kapiga (HK 1) kukutana na waandishi wa habari wa vyombo vya Kikristo kwa ajili ya Kuwapasha habari namna mchakato utakavyoanza na kusonga ili watu wakae mkao wa Kupokea.
             Pastor Harris Kapiga HK 1 akiongea na Waandishi wa Habari wa Media Za Kikristo Siku ya Leo.

Pastor Harris Kapiga amefunguka na kutoa Masharti na Vigezo vya Watu watakaopenda Kushiriki. Vigezo hivyo ambavyo Vitazingatiwa ni kama Ifuatavyo.

1. Awe Ameokoka
2.  Awe Hajatoa Albam Yake Sokoni.
3. Umri Wowote Wa Mshiriki Utaruhusiwa.

Na Vigezo Vingine Vya Ki-Uweledi Vitazingatiwa kwa ajili ya Kutunza nidhamu ya Washiriki Katika Mchakato huo unaotazamiwa kuwa wa Aina Yake.

Akiongea Na Waandishi siku ya Leo Pastor HK 1 amezidi kufunguka kwa kutaja tarehe za Mchakato Katika Jiji na Dar-es-Salaam.
                                                    Sijui Wanafatilia ama Wanasikiliza.

Tarehe 14 April, 2012 Kinyang'anyiro Cha Kuwasaka Washindi katika Kanda Ya Wilaya Ya Temeke Kitafanyika katika Ukumbi wa Saba Saba Opposite na Banda la Maonesho ya Biashara la Ofisi Ya Waziri Mkuu. Mchakato Utaanza Saa 3 Kamili.

Tarehe 21 April, 2012 Jopo la Majaji Litaamia Katika Wilaya Ya Ilala Katika Ukumbi wa Msimbazi Centre Kuanzia Saa 3 Kamili asubuhi Washindi 30 Watakuwa wakitafutwa.
                                                     HK 2 Akiwa katika Pozz la Picha.

Wilaya Inayotabiriwa kuwa na Washiriki Wengi Wilaya Ya Kinondoni Kinyang'anyiro Kitafanyika katika Hotel ya Etina Eneo la Survey Karibu na Mlimani City Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi.

HK 1 ameendelea Kutabanisha Blog hii kwa kusema kuwa Tarehe 2 Mwezi wa May, 2012 Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi Katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Songea, Musoma, Mwanza, Kigoma, Tanga, Arusha na Kilimanjaro. Zoezi la Kuwasaka Nyota Wapya wa Muziki wa Injili litafanyika Kwa mpigo. Mara baada ya Washindi Kupatikana katika mikoa hiyo wataungana na Washindi wa Dar-es-Salaam na Kukaa Kambini kabla ya Kumsaka Mkali Mpya wa Muziki wa Injili Tanzania.
                                                Timu Ya Wanahabari Wakiwa Katika picha ya pamoja

Kinyang'anyiro cha Gospel Star Search litafungwa rasmi 5 August, 2012 katika Jiji la Dar-es-Salaam, ambapo Mzizi Wa Fitina utakatwa siku hiyo.

Kwa Watu Wanaotaka Kushiriki GSS 2012 na Mikoa yao hajatajwa basi wataombwa kushiriki katika Mikoa Jirani.

SOURCE: SAMSALI

Comments