Marvin Sapp ni muimbaji wa Injili anayependwa na kutokana na nyimbo zake zenye kumsifu Mungu album yake ya mwisho kufanya I WIN imemfanya awe na mafanikio na kuinuliwa zaidi. Lakini sasa anaongea na vyombo vya habari kusema anataka kutoa nyimbo za mapenzi kuanzia sasa.
Hivi hii imekaaje? nyimbo za mapenzi zina shida gani zikiimbwa na waimbaji wa injili? Nakumbuka muimbaji wa Injili aliwahi kuimba wimbo mzuri MAISHA YA NDOA kutoka kwenye album yake ya kwanza Jipe moyo. Sikiliza wimbo wa Flora Mbasha