RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WADAU WA RUMAFRICA, BLOGGER WENU RULEA SANGA, LEO JUMAPILI  NASAFIRI KWENDA MBEYA CHUNYA KUMUUGUZA MAMA YANGU.
Ninawaomba wadau wangu kumuombea mama yangu kwani anaumwa sana, mama yangu haongei na hali yake ni mbaya sana. Nauomba kama mdau wangu katika maombi yako ya kila siku mkumbuke mama yangu. 


Nawashukuru walionisaidia katika safari yangu kama Mchungaji Getrude Rwakatare (kwa maombi yako, Mungu akubariki sana mchungaji wangu), Billionaire (kwa mchango wako), Rosemary (kwa mchango wako na maombi yako), Emmanuel Mabisa (kwa ujumbe wako wenye kuleta faraja), Alex Kisonga (kwa faraja zako), Eve wa Double E (kwa moyo wako wa upendo wa kunitembelea nyumbani), Lister (kwa faraja zako, Mungu akubariki), Mzee Scina (kwa mchango wako), Alex (ninaishi naye kwa support yako), Odama (Jennifer Kyaka) kwa mchango wako na maneno ya kunifariji)), Macha (kwa faraja zako), Fadhili Emily wa Fadhaget Santarium Clinic (kwa mchango wako na neno lako la kunifariji) na wengine wengi pamoja na wewe unayepata habari hizi muda huu. Ukitaka kuwasilina na mimi piga +255 715 851523. 

Nakushukuru sana kwa kupoteza muda wako wa kusoma ujumbe huu, Mungu akulipe zaidi ya hapa umetoa katika JINA LA YESU KRISTO 

Nikutakie Ibada njema kwa wale watakao fika kanisani....Nitalimiss kanisa langu la Mlima wa Moto Mikocheni...Sipo kimwili ili kiroho tupo pamoja wana Mikocheni.

Naomba radhi kwa wale wateja wangu, kuwa sitaweza ku-meet deadline yetu ya kazi kutoka na hili lililombele yangu. Ninaamini umenisamehe na samahani kwa kuvunja makubaliano yetu na kuleta hasara katika ofisi yako. Mungu atalipa hilo deni kwa njia zake anazozijua. 
Enzi hizo nikiwa katika kanisa la Nabii TB Joshua, hili ni eneo maarufu kwa jina la Prayer Line ambapo watu wenyeshida mbalimbali huombewa. Leo naomba tushirikiane katika maombi na mahali unapofanyia maombi paweke kama eneo hili la TB Joshua, haya yanafanyika kwa Imani.
Enzi hizo nikielekea kwa Nabii TB Joshua Nigeria, hapa ni Ethiopia. Leo naelekea Mbeya kwa mama yangu Mbeya Chunya kumuuguza mama yangu. Niombee Safari yangu iwe salama. Ninaamini nitafika salaama kwa jina la Yesu Kristo


Comments