Mwandishi: Rulea Sanga
MAONI YANGU, BLOGGER
Mimi kama Rulea Sanga nakumbuka siku ya kwanza kuona misukule ilikuwa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God kwa Mchungaji Getrude Rwakatare na kusikia kuwa Mchungaji Gwajima moja ya maono yake katika kanisa lake ni kupambana na misukule. Katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God ilitokea wakati ibada inaendelea kanisani siku ya Jumapili, mara tukaambiwa kuna vijana wawili wamedondoka kutoka juu ya bati. Watoto hao waliingizwa kanisani na kupelekwa madhabahuni kuombewa na kuhojiwa, imekuwaje wameanguka katika kanisa hilo. Ni story ndefu tuliipata kuhusiana na hao watoto mpaka wakatolewa katika vyombo vya habari
KILICHOTOKEA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B MIAKA YA NYUMA

Watoto wawili pichani aliyelala chini kushoto ni Ramadhani na aliyesimama kulia ni Yusuph. Wanadhaniwa kuwa ni Misukule kulingana na mazingira waliyotokea na wanavyoishi.
Maisha yao ni kufukua makaburi mapya ya watu waliokufa, kuchukua baadhi ya sehemu ya miili kwa matumizi ya chakula(nyama).
Kazi hiyo wanaifanya kwa kutumwa na Bibi yao, watoto hao walidondoshwa na wachawi mchana wa saa nane siku ya Jumapili katika maeneo ya Kanisa la Assemblies of God, Mikocheni B wakati Ibada inaendelea
Msukule Ramadhani yuko chini anatolewa mapepo yaliyomdondosha.
Chini kulia ni Mchungaji Msaidizi Noah Lukumai, katikati ni Mchungaji Chegele na kushoto ni Mzee wa Kanisa Hillary

KILICHOTOKEA LEO IJUMAA-MWANZA
Nyumba ilichomwa moto na kuvunjwa vunjwa.
Nyumba ya bibi Irene iliyo teketezwa leo kwa moto kwa tuuma za uchawi. Bibi huyo ambaye amekuwa akisadikiwa kuwa na tabia ya kuwachukuwa watoto wa majirani zake kwa nguvu ya giza ameumbuka leo baada ya mtoto mmoja aliye potea kwa muda mrefu kwao na kutajwa kuwa alishafariki dunia kisha leo kijana huyo ana kwa ana akakutana na ndugu yake.
Mshangao ulitawala kwa ndugu huyo ambaye kwa ujasili alianza kumuuliza unaishi wapi na kijana yule ndo akamwelekeza kua nipo kwa bibi mmoja anaitwa bibi Irene na tunaishi na wenzangu wengine ambao nilikutana nao pale kwa bibi wakiongezeka siku baada ya siku.
Bibi huyo ambaye anatajwa kuwa mkali katika vitendo vya ushirikina, kakutwa na hilizi kibao na mara baada ya kupata kichapo ambacho hata ivyo akikuonyesha kumdhuru kwa licha ya kupigwa na mawe, bakora na hata vitu vingine vigumu vya hatari hakutokwa na damu, kuvimba nundu wala kuonyesha makovu ya majeraha mwilini mwake, aliwambia wananchi kua watoto wengine wapo ndani na alipo ambiwa awatoe nje alifanya mandingo yake na walio toka ni bata na kuku.

Comments