RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mtungaji wa maswali: Rulea Sanga

SEHEMU YA SABA



Hapa blogger wenu, nilikuwa SCOAN kwa Nabii TB Joshua, eneo hili ni la kupatia chakula. Ukichungulia vizuri utaniona upande wa kushoto wa pili. Naomba ujibu maswali vizuri.


CHEMSHA BONGO NA BIBLE 

Inatusaidie wewe na mimi kuijua Biblia na kumpenda Kristo. Nitakuwa nauliza maswali katika kitabu  fulani, kwa mfano mwezi huu wa Julai tutakuwa tunaulizana maswali katika kitabu cha MATHAYO na mwezi unaofuta itakuwa kutoka katika kitabu kingine.

Mwisho wa mwezi kutakuwa na mtihani ambao utaufanya bila ya kuangalia katika Biblia yako. Ninaamini wewe umeokoka kwahiyo hutaweza kunidanganya kwa kuangalizia katika Biblia.


NB: Naomba usiangalie majibu kabla hujajibu kutoka katika akili yako:


MASWALI KUTOKA KATIKA KITABU CHA MATHAYO 17 MPAKA MATHAYO 19

  1. Mama yao na Zebedayo alipomwendea Yesu na kutaka wanae wawili wakae mmoja mkuno wa kuume na mwingine mkono wa kushoto katika ufalme wake Yesu.

    (i) Yesu alimjibu nini huyo mama?

    (ii) Yesu alimpomjibu yule mama na kumuuliza, Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?. Huyo mama alimjibuje?

    (iii) Ni nini Yesu aliwaambia baada ya you mama kumjibu Yesu?
  2. (i) Ni walemavu wa aina gain waliokaa kando ya njia, nao waliposikia Yesu anapita wakapaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana wa Daudi!?

    (ii) Baada ya Yesu kusikia sauti ya hao walemavu, aliwambia nini?

    (iii) Hao walemavu walipoambiwa na Yesu kitu gani awafanyie, unafikiri aliwajibu nini, na walitatuliwa tatizo lao. Na kama walitauliwa tatizo lao,  Yesu alitumia njia gain kuwaponya ?
  3. Ni baada ya kufanya nini, Yesu aliwaambia, “Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.
  4. (i) Kwanini Yesu aliuambia mti unyaeke na yasipatikane matunda milele na baadae mti ukanyauka?

    (ii) wanafunzi wa Yesu baada ya kuona mti umenyauka mara moja, walistajabu sana. Yesu aliwaambia ni wanafunzi kuhusiana na mti huo kunyauka?
  5. Unampenda Yesu? Kama unampenda ni kitu gain utafanya leo kuonyesha unampenda Yesu?

MAJIBU
  1. (i) hamjui mnaloliomba (Mathayo 20:22)

    (ii) twaweza (Mathayo 20:22)

    (iii)  Hakika mtanyea kikombe changu, lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari, na Baba yangu (Mathayo 20:23)
  2. (i) vipofu wawili. (Mathayo 20:30)

    (ii) mnataka niwafanyie nini? (Mathayo 20:32)

    (iii)  walisema, Bwana twataka macho yetu yafumbuliwe. Tatizo lao lilitatuliwa baada ya Yesu kuwagusa macho yao, nao wakamfuata (Mathayo 20:32)
  3. Ni baada ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao waliokuwa wanauzia njiwa (Mathayo 21:12)
  4. (i) Kwasababu Yesu aliposikia njaa na kuusogelea ule, na mti haukuwa na matunda (Mathayo 21:18)

    (ii) akasema “Amini, nawambia mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya sio hili la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yoyote mtakayoomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Mathayo 21:21)
      5. Hakuna jibu..jibu uliojibu ni sahihi kwako

MUNGU AKUBARIKI. KESHO TUANENDELEA KUANZIA MATHAYO 20 NA KUENDELEA>

Comments