RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FRIENDS ON FRIDAY KUFANYIKA MBEYA IJUMAA YA LEO-MCHEKESHAJI CHAVALA KUHUDHULIA SIKU HII

Mwandishi wenu: Rulea Sanga

Kutokana na taarifa nilizozipata blogger wenu, (Rulea Sanga) ni kwamba mashamsha ya kumtukuza Mungu yanaendelea usiku huu katika hotel ya Metro Cuisine-Mbeya.


Mashamsham haya ufanyika kila mwisho wa mwezi ambapo wampendao Kristo hukusanyika pamoja na kupata burudani mbalimbali kama vichekesho, uimbaji, taarifa mbalimbali, kujuana, kubadilishana mawazo.

Hii ni moja ya mitoko ya wapendwa, kwamaana hatuwezi kwenda disco au bar, ila kwa kupitia FOF tunapata sehemu ya kukutana na kumtukuza Mungu

MSHIRIKI

Aica Sasali 
BANGO LA HOTEL
Bango la Hotel

MC WA LEO
 
Clemence Kabuje.

BAADHI YA WADAU



USHAURI KUTOKA KWA RULEA SANGA

watu wa Mungu kuna jambo ambalo mimi huwa nakereka sana kwenu Watanzania ambao tunajiita tumeokoka. Kero yangu kubwa ni kwamba hatutaki kuwa mashabiki wa mambo ya Mungu. 
Kila jambo linapotokea tunakuwa goigoi sana. Tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kushabikia ya Mungu.

Utaona kuna mkutano umeandaliwa na watumishi wa Mungu kwa pesa nyingi sana, lakini sisi hatufiki kuwa-support na kusikiliza ujumbe kutoka kwa Mungu. Kumbuka hawa watumishi ndio Mungu anawatumia kuleta ujumbe wake kutoka mbinguni ili sisi tuishi kama anavyotaka.

Mbali na watumishi kuandaa mikutano, pia kuna watu wanaandaa matamsha kwaajili ya kumsifu Mungu kwa nia ya uimbaji. Kumbukeni Mungu anapenda sana sifa, sasa wewe unapokosa kuja kumsifu Mungu pamoja kwa umoja unategemea nani aje amsifu Mungu wetu. Mimi nakuomba wewe uliyebahatika kusoma ujumbe huu, uwe ni mshabiki wa kazi ya Mungu

Angalia watu wa mataifa wanavyopenda mambo yao. hapa Tanzania kuliakuwa na kitu kinaitwa DAR LIVE, watu walikuwa wanajaa sana kwenda kuangalia waimbaji kama Diamond, Ali Kiba, Twanga Pepeta, Mwasite, Rinah sanga na wengine wengi. Hii inaonyesha kuwa wanapenda mambo yao ya kidunia kwa moyo wa dhati, na wapo tayari kuwa-support kwa gharama yoyote ile.

Watanzania hebu tuone aibu kushindana na hawa watu wa mataifa. Tushikamane na tuache udini , tufanye kazi ya Mungu. Sisi tunatakiwa kuonyesha mfano kwa mataifa na kutoa ushuhuda kuwa kweli mambo ya Yesu ni balaaa.

Jipange kaka yangu, dada yangu, baba, yangu, rafiki yangu, mdogo wangu.

Nakuomba msamaha kama nimekukwaza

Pia naomba maoni yako, kwanini hatupendi kwenda kwenye mikutano na matamsha?

Comments