Mwandishi: Rulea Sanga
Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B linakukaribisha katika ibada itakayofanyika siku ya Jumapili kanisani hapo. Mchungaji Getrude Rwakatare anakukaribisha anasema, "Njoo umtukuze Mungu na Mungu afanye baraka kwako". Pia kutakuwa na maombi ya kudondosha ngome za adui shetani. Kumbuka kuja kwako kanisani ni uamuzi wako, ila la msingi ni kujua kuwa Mungu anakuhitaji sana katika ufalme wake.

Mchungaji Mh. Dr. Getrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblie of God.
Katika ibada hii kutakuwa na Neno la Mungu, ambapo kutapamwa na uimbaji kutoka kwa Neema Jekonia , Joys Bringers na Happy kwaya.
Jitahidi kufika na Mungu akuwezeshe uje na rafiki yako au ndugu yako.
Ibada itaanza saa 3:00 asubuhi na kuendelea.

Mchungaji Rwakatare akiombewa
Kama ni mgeni, panda magari ya Mwenge, na ukifika hapo utaona kuna bajaji nyingi, uliza kanisa la Mchungaji Mama Rwakatare. Pia kuna mabasi ya St. Marys's ambayo yatakuleta kanisani bila ya nauli yoyote.
MUNGU AKUBARIKI

Comments