RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA ASHANGAZWA NA KANISA LA EFATHA MWENGE


Mwandishi: Rulea Sanga

Blogger wenu (Rulea Sanga) Ningependa ku-share na wewe yale niliyoyapata katika kanisa la EFATHA Mwenge Dar es Salaam kwa Mtume na Nabii Josephat Mwingira. Namshukuru Mungu kwa kunisukuma siku ya Jumapili na kuudhuria ibada iliyokuwa inaendelea katika kanisa hilo. Nilibahatika kuhudhuria ibada ya pili ambayo kwa kawaida inaaanza mida ya saa 4:00 asubuhi, ila mimi nilifika mida ya saa 5:30 asubuhi. Kuna mambo mengi nilijifunza katika kanisa lile na kuona kumbe watu wa Mungu wamaweza kufanya vitu vizuri sana wakiamua. Vitu amabvyo vilinistajabisha na kuutakasa moyo yangu ni kama vifitavyo:

Mtume na Nabii Josephat Mwingira Kushoto akiwa na Nabii TB Joshua


  1. MUONEKANO WA KANISA
    Kanisa limejengwa katika ramani ya kisasa kabisa, rangi zao walizotumia zinaleta utukufu ukiziangalia. Kanisa ni kubwa sana. Limejengwa kiasi kwamba ukiwa ndani hupati joto , kuna hewa ya kutosha ambapo hujisikii jasho kabisa. Kilichonifurahisha ni kuona ndani ya kanisa kuna samaki zinafugwa na ni nyingi sana. Madhabahu ni kubwa mno na imepambwa vizuri sana.

    Kanisa limezungukwwa na TV zinazosaidia hata mtu aliyekaa mbali anaweza kuona kinachoendelea madhabahuni.

    Eneo la mbele ambako kuna parking ya magari

  2. MUDA WA KUINGIA KANISANI
    Mimi nilifika pale nimechelewa, na nikazuiliwa kuingia kwani kilikuwa kipindi cha maombi. Nikajifunza kuwa watu wanapokuwa wanamtafuta Mungu hawapendi kuona kuna mtu au kitu ambacho kinaweza kuwavurugia mawasiliano na Mungu. Baada ya maombi kuisha niliruhusiwa kuingia.

    Waumini wakitoka ibada ya kwanza
  3. UTARATIBU WA IBADA
    Ukiingia ndani ya kanisa, waumini wamekaa kimakundi (Zone) nikimaanisha watu wanaotoka eneo fulani wanakaa pamoja. Hii inasaidia kutambua na kujua kama kuna mtu hajafika kanisani kumfuatilia. Au kama anaumwa ni rahisi kumsaidia. Katika makundi hayo kunakuwa na utaratibu wa kupitisha karatasi la kuandika majina kwa wale waliofika. Nilifurahi sana.

    Pale mbele ndio madhabahu. Waumini wakiwa katika mkao wa ki-zone
  4. UIMBAJI
    Kwaya zao zimejipanga vizuri kisauti, kimavazi na uchezaji wao unapendeza kiukweli. Wanapoimba unahisi uwepo wa Mungu unashuka. Discipline imetawala katika kwaya zao. Wamejipanga vizuri sana kiuimbaji.
    Kuna kipindi hamrusiwi kucheza nyimbo, bali waimbaji tu wanakuwa wanaimba. Hii inaashiria kuwa watu wanatakiwa kusikiliza ujumbe unaotoka kwa waimbaji. Na baada ya muda Fulani kunakuwa na nyimbo za kushirikiana kuimba na kucheza.


    Music System iko safi sana, unapata stereo ya hali ya juu. Unapowasikiliza waimbaji unakuwa kama unasikiliza CD katika radio yako. Kila kifaa kinasikia kwa kiwango cha hali ya juu sana.

  5. UTOAJI WA ZAKA NA SADAKA
    Kuna utaratibu mzuri sana na ni heshima mbele za Mungu. Wahudumu wanagawa bahasha ambazo zimeprintiwa deatail za kanisa na kila sadaka ina bahasha yake maalum. Tofauti na sehemu zingime ambapo watu wanaenda kumtolea Mungu sadaka kama wanaenda kutupa pesa kwa kuikunja noti mpka unaionea huruma.

  6. MATANGAZO
    Matangzao yao yamerekodiwa, kwahiyo watu wote mnakaa kimia mnasikiliza kile kinachotoka katika radio. Kama kunatangazo la ghafla basi mhusika atatangaza madhabahuni
  7. PROJECTS/MIRADI
    Kanisa hili mbali na kuwa limejikita katika kumtangaza Kristo lakini lina miradi mbalimbali. Baadhi ya miradi yao ni:
·         NURU INSUARANCE- Ni kampuni ya Bima inayoendeshwa na kanisa la Eaftha Mwenge.

Watu waliombwa kujiunga na BIMA hii na kuunga nkono kazi ya Mungu. Huduma hii huanza saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni. Umefika wakati wa kupenda vya Mungu ambavyo vinatolewa na watumishi wa Mungu.Wafanyakazi wa Nuru Insuarance wako tayari kukufuata mahali ulipo.

·         EFATHA BANK- Kanisa la Efatha linamiliki Bank. Uomgozi uliwaomba watu waweze kuweka fedha zao katika Bank hiyo na kununua hisa

·         TRENET TV. Pia Mungu amewawezesha kumiliki TV yao ambayo siku ya Jumapili hurusha ibada inayoendelea katika kanisa hilo. Na siku zingine kunakuwa na matangazo mbalimbali

Unaweza kuwasiliana na aknisa hili kwa
Simu +255 22 2773 535 B/Pepe efatha2001@yahoo.com


MTUME NA NABII JOSEPHAT MWINGIRA ALIHUBIRI JUU YA NGUVU ZA MUNGU KAMA MUENDELEZO WA IBADA ZILIZOPITA

Nabii Josephat Mwingira alianza na kutueleza sababu za Walokole wengi kuwa maskini, naye alitoa sababu tatu nazo ni:
  1. Hawashiki utakatifu
  2. Hawalindi Imani yao
  3. Hawajawa mashahidi wa Mungu
Nabii Mwingira alitoa siri za kufanikiwa
  1. Ukifanya kazi na Mungu na kwa kufanya yaliyo mema (Warumi 8:8)
  2. Kubarikiwa rohoni. Roho yako kama imebarikiwa na Mungu utaona mafanikio. Mungu ataibariki roho yako kama wewe mwenyewe ni msafi kiroho
  3. Kufanikiwa kwa roho yako. Roho yako ikifanikiwa utakula mema ya dunia
  4. Kumtukuza Yeye awezaye kutuwezesha sisi kufanya mambo yote kuliko tunayoomba (Efeso 3)
  5. Kufanya kazi kwa nguvu yako yote na akili yako yote (Yohana 14)
  6. Kupiga vita vizuri vya imani (kupigania imani yako) Pasipo imani huwezi kumpendeza  Mungu
  7. Kumpendeza Mungu kwa kutii
  8. kushika uzima wa milele ndani yako, kwa kuishi maisha matakatifu
  9. Kujifunza kuwa mkweli
  10. Ungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi
Nabii Josephat Mwingira anasema aliposhika hayo yote hapo juu alikusahau yote ya dunia na kuona ni mavi (Wafilipi 3:8)

MUNGU IBARIKI HUDUMA YA EFATHA
AMENI




Comments