RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMA AFRICA INAWAPONGEZA KANISA VICTORY CHRISTIAN CENTER (VCC) KWA KUPATA HEMA JIPYA KWAAJILI YA YESU KRISTO


RUMA AFRICA inawapongeza kwa kazi nzuri ambayo mmeifanya kwa utukufu wa Mungu Baba aliye mbinguni. Ni kazi nzito mmeifanya lakini tunatambua ni kwa neema ya Mungu. Kuna makanisa magapi hapa Tanzania ni ya miaka nenda rudi na makubwa lakini maendele ni madogo sana. Makanisa hayabadiliki yanazidi kuwa machakavu na sadaka zinakusanywa nyingi sana. Kitendo hiki wana RUMA AFRICA huwa kinatusikitisha sana. Tujaribu kufanya kazi ya Mungu ikapendeza machoni pa watu na mbele za Mungu. Majumba yetu binafsi tumejenga yanapendeza sana lakini nyumba ya Mungu inakuwa kama jumba la kuifadhia mizigo. Watumishi wa Mungu umefika wakati wa kufuata mifano ya makanisa haya ambayo mimi kama Mkurugenzi wa RUMA AFRICA nimeyaona hapa jijini Dar es Salaam, VCC na CCC la Upanga Dar es Salaam. kama wao wameweza sis tushindwe tuna nini?.

  Mtumishi Wa Mungu Rev. Dr. Huruma Nkone akiwa Kwenye Prayers Kwa Kumshukuru Mungu.

Mungu anapenda na Yeye kuona kazi yake hapa duniani inakuwa mfano kwa mataifa na watoto wake wanakaa katika mazingira mazuri. Vitu vizuri ni vya Mungu na vibaya ni vya shetani. Mnisamehe kama nimewakwaza watumishi wa Mungu.

Hongereni sana VCC Mungu wangu awabariki na abariki kazi ya mikono yenu. Nakupongeza Brother Sam Sasali kwa kutupigia hizi picha na leo mataifa wanaona maendeleo ya kazi ya Mungu.
                                                    Dr. Rev. Huruma Nkone Ndani Ya Ibada

Kanisa la VCCT lililo chini ya Rev. Dr. Huruma Nkone siku ya Jumapili ya tarehe 29 July, 2012 wamefanya Ibada ya Shukrani ndani ya Hema Mpya Ya Kisasa ambayo imeagizwa Kutoka South Africa maalum kwa Ajili Ya Ibada.

Hema Hiyo Ya Kisasa yenye uwezo wa Kuchukua Watu takribani 1000 kwa Mara Moja imefungwa katika Kiwanja Cha Kanisa hilo kilicho maeneo ya Mbezi Beach Kawe ambapo Kwa maelezo ya Dr. Huruma Nkone Hema hiyo ni ya Muda Kabla Kanisa halijaanza Ujenzi wa Kanisa Kubwa la Kisasa ambalo litaitwa VCCS-- Victory Christian Centre Sanctuary.
                                Tabernacle Inavyoonekana Kwa Nje, Hapa Watu wakianza Kufika 
Kwa Karibu zaidi

Ibada ya Jana ambayo ilikuwa Maalum kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa kuwafikisha hatua hiyo ilifanyika ndani ya Hema hiyo Ya Kisasa. Ndani Ya Kanisa hilo,  Kanisa Zima zileweka Zuria la Kisasa lenye Kunyonya Mawimbi Ya Sauti Kwa ajili Ya Vyombo Vya Muziki kwa ajili ya Kuzuia Mwangwi, Ndani ya Hema hiyo kimefungwa Chomo Maalum Cha Kudhibiti Sauti Ili Sauti Isisumbue Majirani ( Sound Proof), Ndani Ya Hema Hilo Limezunguzwa na AC, Viyoyozi Vya Kisasa kwa ajili ya Kuhifadhi ubaridi wakati wa Ibada na Kuondoa Joto, Milango Ya Kanisa hilo ambayo inategemewa Kuwekwa Mwanzoni Mwa mwezi wa 8 ni Milango Ile Maalum "Automatic Doors" ambapo zitakuwa ikifunguka yenyewe Kadri Washirika Watakavyokuwa Wakiingia, mbali na hayo Sound System iliyofungwa ni madhubuti kwa ajili ya hema hiyo.
Hapa Vijana wakifanya Set Up Ya Venue kwa ajili ya Ibada Viti Vyekundu Ni Maalum kwa Ajili ya Hema.
                                    Carpet Maalum kwa ajili ya Kuzia Mwangwi Wa Sauti
                                                                        Ndani Ya Hema

Mzee Kiongozi Wa Kanisa la VCCT Dr. Eda Wandwi akiongea siku Ya Jana Katika Ibada hiyo amesema Kanisa lina Maono Ya Kununua Mabasi yatakayokuwa Yakiwachukua Washirika wa Kanisa Hilo Katika Vituo Maalum na Kuwapeleka Kanisani hapo Kila siku Ya Ibada.

Kanisa la VCCT ambalo liko chini ya Dr. Huruma Nkone, asilimia 60 ya Washirika Wa kanisa Hilo ni Wanafunzi, na Asilimila 80-85 Ya Washirika ni Vijana. Kati Ya Vitu ambavyo Dr. Huruma Nkone ame invest katika Kanisa hilo ni
                                                The Rivers Of Joy Wakienda Sawa

1. "Quality"---- Katika hili Designing Ya Kanisa aliibuni Pastor Mwenyewe, Events za Kanisa kama Campus  Night, Soul Breakfast, Open Mic Open heart na Zingine ni Za Kiwango Kikubwa.
                                                 Pastor Huruma and Pastor Joyce Nkone

2. Raising People's Talents---- Dr. Huruma Nkone amejaaliwa Karama ya Kugundua, Kulea na Kuendeleza Talents Za Watu, The Praise Team, Ushers Organisation, Mcz, teachings, Singing unless mtu hajataka Kutumika lakini yeyote aliye tayari Kutumika Mlango Uko Wazi. Kwa Sasa imeanzishwa Praise Team (Rivers Of Joy Junior) ambayo hii ita raise Praise and Worship Leaders Miaka 10 Ijayo ambao Kwa sasa wako katika professional teachings.
                                                                     Kitu Sebeneeeee
3. PFW---Prayer, Fasting and Word Of God---- Ni Lazima Kila Mwezi  Wiki ya Kwanza Utaratibu wa Kanisa Washirika Kufunga na Kuomba Kama Kanisa, na Kuna Maombi Alfajiri, Mchana na jioni, Kila Mwanzo Wa Mwezi Wiki ya Kwanza ni YA Mungu. Washirika Wamegawiwa katika Vikundi Mbalimbali wanakokaa, Vijana, Wanawake, Wanafunzi Kila Jumamosi Ya Mwisho wa Mwezi, Wana taalum kila Mwanzo Wa Mwezi Jumapili, hakuna Kada mbayo imeachwa bila watu wa aina hiyo Kukutana Kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu.
                      ndani ya Ibada Kukawa kuna dakika 10 za Ku Network na Kusalimiana

Kwa
 Juu kwa Nyuma ni Amani Kapama Mpiga drums, Kwenye Mic ni Sarah Shilla ndani ya Praise Team


                                                                Full Technology ndani ya Kanisa.
                                                             Worship Moment
 Professional Sound Engineer and Songs Writer Raphael akiwa Kikazi Zaidi.
 Pastor akiteta Jambo ndani ya Ibada ndani ya dakika Kumi za Ku Network.
Jana Mise alifunika sana na Hii Kitu Saxerphone, Kuna Shule maalum inaanza Mwezi huu kwa ajili ya kufundisha kupiga hii kitu.

Mawasiliano ya Mtandao....www.vcc.or.tz kwenye facebook Page ya Kanisa inaitwa, "Victory Christian Centre (VCC)", Page ya Vijana Inaitwa "The Bridge Youth Ministry" na Page Ya Wanafunzi inaitwa "Soul Breakfast"

Comments