RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMA AFRICA YAIPONGEZA FOF YA MBEYA NA ARUSHA KWA KAZI WALIYOFANYA IJUMAA

Mwandishi: Rulea Sanga

RUMA AFRICA inawapa pongezi kubwa sana kwa wapenzi wa FOF kwa zoezi lao kubwa la kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji, vichekesho na pia kujuana wapendwa kwa wapendwa. Tumefurahi sana na Mungu azidi kuibariki FOF kwa juhudi zake. Mungu awalinde wabeba maono na waanzilishi wa FOF Tanzania na kuwapa ubunifu zaidi.

Kutoka na taarifa tulizopata kutoka katika mitandao mbalimbali wanasema FOF ya mwezi huu ilikuwa babu kubwa sana, watu walibarikiwa sana kimwili na kiroho. Tumeambiwa kulikuwa na mishikaki ya kutosha na vinywaji vingi. Pia Neno la Mungu halikukosekana mahali pale.

Wadau wa FOF walipata mishikaki

FOF inazidi kupaa na kuendelea mbele.

RUMA AFRICA bado iko katika kilio chake kwako wewe ambaye hupendi ku-support kazi ya Mungu. Watu wanatumia fedha zao na akili zao kukuandalia mazingira kwaajili yako wewe kuja kumtukuza Mungu, lakini cha kusikitisha hufiki. Tunakuomba unaposikia kuwa kuna mikutano au matamsha, hudhuria basi ili kazi ya Mungu isonge mbele. Kama ni kijana ni wakati wako wa kufanya kazi ya Mungu, ukizeeka utakuwa na majukumu mengi ya kifamilia na utakosa hata muda wakufika katika matamasha. Vijana changamkeni kufanya kazi ya Mungu. Kuweni wabunifu kwa kuleta vitu vipya tena ikiwezekana zaidi ya FOF

Ngoja tuone kilichotokea huko Mbeya

Wanambeya Bwana asifiwe


"Tunashukuru FOF, leo mashavu lazima yarudi katika hali yake ya kawaida" Mchekesahaji Chavala (kulia) akipata chakula cha nguvu


Mchungaji Matty kulia akiteta jambo na mdau wa FOF


Pozz la Kwaito


Ze comedian Cahvala akifanya vitu vyake

Dancing Time FoF Arusha
Hii ni Mojawapo ya groups zikishiriki michezo ndani ya FoF


Vipi mpiga picha nikuachie kipande...?

Bavuma Sijui ndo alikuwa asimamizi ama anadokoa


Band Ikienda Sawa

Comments