Mtunzi wa mtihani: Rulea Sanga
Tafadhari
jibu maswali bila ya kuangalia majibu, na baada ya kuyajibu yafananishe na yale
uliyopewa na RUMA Africa
MASWALI YANATOKA KATIKA KITABU CHA MARKO.
MASWALI
- (i) Yesu alisema nini kuhusiana nyumba yake alipokuta watu wakiuza na kununua
ndani ya hekalu huko Yerusalem na kuamua kuwafukuza ?
(ii) Kwanini wakuu na makuhani walimuogopa Yesu alipowafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu huko Yerusalem?
- (i) Yesu alisemaje kuhusu imani kwa wanafunzi wake walipoona mti alioulaani ukiwa umenyauka?
(ii) Faida gani ambazo zinatokana na kusali alizozitamka Yesu kwa wanafunzi wake ?
- (i) Yesu alimjibu nini Pilato
baada ya kufungwa na wakuu wa makuhani pale alipoulizwa, “Ndiwe mfalme wa
Wayahudi?”
(ii) Je, Yesu aliendelea kumjibu Pilato alipokuwa anaulizwa maswali baada ya kujibu lile swali la “Ndiwe mfalme wa Wayahudi?”
(iii) Kama ilivyo desturi wafuasi wa Pilato au makutano, wakati wa sikukuu hufunguliwa mfungwa mmoja tu.
(a) Makutano walimuomba nani afunguliwe?
(b) Kwanini makutano hwakutaka kumfungulia Yesu?
(c) Kwanini Pilato aliwauliza makutao, “Je, mnataka mfalme wa Wayahudi (Yesu)”?
(d) Makutano walimjibu nini Pilato baada ya kuuliza makutano, nimtendeje huyu mnayenena kuwa ni mfalme wa Wayahudi?
MAJIBU
- (i) Yesu alisema nyumba yake ni nyumba ya
sala kwa mataifa yote (Marko 11:17)
(ii) Wakuu na makuhani walimuogopa Yesu kutoka mkutano wote walishangaa kwa mafundisho yake. (Marko 1118) - (i) Yesu aliwaambia amini,
nawambia, Yeyote atakaye uambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala
asione shaka moyoni mwake, ila amini kwamba hayo asemayo yametukia (Marko
11:23
(ii) Faida za kusali
(a) Yesu aliwambia wanafunzi wake, yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
(b) Nanyi msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neon juu ya mtu, ili na Baba yenu wa mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu wa mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
(Marko 11:24-26)
- (i) Yesu akamjibu, “Wewe
wasema” (Marko 15:2)
(ii) Yesu hakujibu neon tena, hata Pilato akastajabu (Marko 15:5)
(iii) Walimuomba afunguliwe
(a)Baraba (Marko 15:11)
(b)
(c) Kwasababu Pilato alitambua ya kuwa wakuu wa makuhani wamemtoa kwa husuda. (Marko 15:12)
(d) Msulubishe (Marko 15:13)
Comments