Mwandishi: Rulea Sanga
Muache Mungu aitwe Mungu, unaweza kujiuliza kwanini Mungu alimuumba huyu mtoto akiwa na hali kama hii, na baada ya masaa sita kumchukua tena? Kumbuka mama wa huyu mtoto ametunza mimba ya huyo mwanae kwa muda wa miezi tisa tumboni mwake, na amevumilia mateso yote. Kingine cha kujiuliza ni kwanini leo hii umebahatika kuiona hii picha na hukubahatika kumuona huyu mtoto LIVE akiwa duniani?
Nadhani kuna jambo Mungu anataka ujifunze kupitia huyu marehemu. Nilikuwa najiangalia sura yangu na kuiona iko poa sana na inavutia sana mbele za watu. Nimekuwa nikiuangalia umri wangu na kuona nimeishi muda mrefu sana toka nizaliwe. LAKINI nikawa najiuliza ni kazi gani nimeifanya kumtangaza KRISTO kutokana na uzuri nilionao? Nikaona na sijafanya lolote nikilinganisha na umri wangu, na nimekuwa mtu wa kupokea kutoka kwa watumishi wa Mungu katika mikutano au makanisani. Nikajiuliza tena, toka nimezaliwa nimewaleta watu wangapi kwa Yesu? Jibu langu likawa na kigugumizi sana, nikaona ni wachache sana ukilinganisha na umri wangu. Tatizo ni nini?
Yesu akiwa na umri kama wangu aliwaokoa watu wengi sana na kufanya miujiza mingi sana kwa watu, lakini mimi na umri wangu huu sijafanya hivyo, ni kwanini?. Yesu alisema sisi tutafanya makubwa zaidi ya aliyoyafanya, lakini mimi bado sijafanya, kwanini?
Huyu mtoto ametufundisha mengi sana...mimi sitaki kukueleza mafunzo tunayopata kutoka kwa mtoto huyu ambaye kwa sasa hayuko duniani. Jilinganishe wewe na mtoto huyu, na "assume" wewe ungekuwa ndio huyu mtoto na huyo mtoto angekuwa ndio wewe, ungejisikiaje? Urembo wangu bila ya kuwa na Mungu ni kazi bure na ni mateso duniani
Nahisi kulia kwa kuona uzembe ninaofanya katika kazi ya Mungu. Ee Mungu nisaidie nikutumikie kwa kupitia karama na kipawa ulichonipa cha blogu. Naomba watu waje kwako kwa kupitia vile naviweka katika blogu hii. Wape ufahamu wadau wangu wakupende wewe Mungu. Wasaidie ili nao wawasaidie wenye uhitaji na kiu ya Neno lako.. Tuepushe na majivuno kutokana na uzuri wa sura zetu na mali zetu. Mungu tukutumikie wewe..Nimeomba kwa jina la Yesu Amina
Mtoto
azaliwa na vichwa viwili katika hospital ya DDH Bunda Mara mtoto huyu
alikaa kwa saa moja ni kisha kufariki dunia picha imepigwa na Berensi Alikadi mshiriki
wa mafunzo ya Online Journalism yanayoendelea Mkoani Mara , Mafunzo
hayo yanayoendeshwa na Mkufunzi Msaidizi Mkami Jr Kutoka Mjengwa Blog ,
Yakiratibiwa na UTPC
Comments