Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania akizungumza. |
Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini
kuacha kuwa chanzo cha migogoro makanisani na badala yake kurudi zaidi
kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza kusudi walilopewa katika utumishi
wao.
Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa
miaka hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union)
zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya
Muhimbili wakati alipohudhulia kama mgeni rasmi wa tukio hilo.
Alisema tatizo kubwa lilipo makanisani kwa hivi sasa linasababishwa na
viongozi wenyewe ambao badala ya kumtumikia Mungu wamegeuka na kuangalia
vyeo hivyo basi ni vyema kurudi kwa Bwana ili waweze kumtumikia.
“Migogoro mingi iliyopo makanisani hivi sasa matatizo makubwa yako
kwenye uongozi wala sio wanaoongozwa cha muhimu tu ni kwamba viongozi
warudi zaidi kwa Bwana wanayemtumikia” alisema Jaji Augustino Ramadhani.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Jaji Angera
Kileo, Askofu Philemon Tibanenason, Mweka Hazina wa Chuo Kikuu cha
Mlimani, Donata Mugassa pamoja na viongozi wa shirika hilo, Mwenyekiti
Dk. Edda Mwandi aliyekuwa mwenyeji wa sherehe hizo pamoja na Katibu Rev.
Emaus Bandikile.
source--gospelvisiontz.blog
Comments