RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE



MTUNZI: Rulea Sanga
ONYO: Tafadhali usiangalie majibu kabla ya kujibu kwa kutumia akilia yako

MASWALI
  1. (a) Kwanini Mafarisayo walitaka kumvizia Yesu katika Sinagogi kwa kutaka amponye mtu ambaye aliyepooza mkono wake wa kuume siku ya sabato.

    (b) Baada ya Yesu kuona mawazo ya Mafarisayo kuhusu kumponya mtu aliyepooza mkono wake wa kuume, alimwambia nini kwa huyo aliyepooza

    (c) Yesu aliwaambiaje Mafarisayo kuhusiana na alivyomponya mtu aliyepooza mkono wake wa kuume katikaSinagogi?

    (d) Je, Yesu alimponya yule mtu aliyepooza mkono wake wa kuume?

  2. Yesu aliporudi kutoka mlimani ambako alikuwa akioomba na kukesha usiku kucha, ni kwanini makutano walitaka kumgusa?

  3. Malizia misemo ya Bwana Yesu aliyosema kwa wanafunzi wake:

    (a) Heri ninyi mlio na njaa-------------------------------------

    (b) heri ninyi mliao sasa----------------------------------------

    (c) Heri ninyi watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu na kulitupa nje jina lenu kama neon ovu kwaajili ya Mwana wa Adam---------------------------------------------------

    (d) Ole wenu mlio na mali, kwa kuwa--------------------------------------

    (e) Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa kwa kuwa-------------------------

    (f) Ole wenu ninyi mnaocheka kwa kuwa-------------------------------------

  4. Yesu alisemaje kwa wale ambao wanaotuchukia au adui zetu?

  5. Yesu anasema tufanye nini kwa wale
    (a) Wanaotulaani

    (b) Watupigao shavu moja

    (c) Watunyang’anyao majoho yetu

    (d) Watuombao

    (e) Watunyang’anyao vitu vyetu

MAJIBU
  1. (a) Walitaka kumshitaki (Luka 6:7)

    (b) Ondoka, simama katikati (Luka 6:8)

    (c) Je, ni halali siku ya Sababto kutenda mema au kutenda mabaya; kuponya roho au kunyamaza? (Luka 6:9)

    (d) Yesu aliwakaza macho, akawaambia, “Nyoosha mkono wako, akanyoosha mkono wake akawa mzima tena (Luka 6:10)

  2. Kwasababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote (Luka 6:19)

  3. (a) kwasababu mtashibishwa

    (b) kwasababu mtacheka

    (c) 

    (d) faraja yenu mmekwisha kuipata

    (e) mtaona njaa

    (f) mtabembelezwa

    (Luka 6:20-26)

  4. Tuwapende (Luka 6:27)

  5. (a) Tuwabariki (Luka 6:28)

    (b) Tuwageuzie shavu la pili (Luka 6:29)

    (c) Tusiwazuilie (Luka 6:29)

    (d) Tuwape kile watuombacho (Luka 6:30)

    (e) Tusitake waturudishie (Luka 6:30)

Comments